Mnangagwa amesema uchaguzi uko palepale
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa tarehe 30 mwezi Julai, ingawa kulitokea alichokiita jaribio la kukatiza uhai wake lililotokea siku ya Jumamosi.
Katika hatua nyingine, msemaji wa Polisi, Charity Charamba amevitaka vyombo vya habari na Umma kujitokeza iwapo wana picha za video za tukio la mlipuko wakati huu ambapo uchunguzi unafanyika.
Amwewaambia wanahabari mjini Harare kuwa zawadi nono itatolewa kwa taarifa itakayotolewa kusaidia kwenye uchunguzi wao.Idadi ya waliojeruhiwa sasa imefika 49 na Polisi na idara za usalama ziko katika uwanja wa White City eneo ambalo mlipuko ulitokea.
Watu walijeruhiwa kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mkutano wa hadhara mjini Bulawayo, tukio lililotokea karibu kabisa na Mnangagwa wakati akiondoka jukwaani.
Maafisa wamesema masuala ya usalama yataangaliwa tena.
mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa ni wa kwanza tangu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kuondolewa madarakani na kurithiwa na Mnangagwa.
Mnangagwa alisema kuwa mlipuko ulitokea baada ya kitu ''kulipuka hatua chache na nilipokuwa-lakini muda wangu haujafika''.
amesema kuwa ghasia hazina maana na ametoa wito wa kuwepo umoja.
Kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa pia amekemea shambulio hilo,akisema kuwa machafuko ya kisiasa ''hayakubaliki''.
Waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo ni pamoja na makamu wa rais wawili, Mwenyekiti wa Chama cha Zanu-PF, wanahabari wa Televisheni ya taifa na maafisa wa usalama.
Rais wa nchi hiyo alikuwa mjini Bulawayo, mji wa pili wa nchini humo na ngome ya upinzani, kwa ajili ya kufanya kampeni kwa ajili ya chama chake cha Zanu-PF wakelekea kwenye uchaguzi wa mwezi Julai
Maoni