Mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea walikuwa wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili Lukaku lakini badala yake akajiunga na Manchester United.
Mshambuliaji Romelu Lukaku aliamua kuondoka Everton baada ya ujumbe wa ''uchawi'' kumwambia ajiunge na Chelsea kulingana na mwenye hisa mkuu wa klabu ya Everton.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 baadaye alijiunga na Manchester United kwa dau la pauni milioni 75 msimu wa uhamisho uliopita.
Farhad Moshiri aliwaambia wenye hisa katika mkutano na wachezaji kwamba mchezaji huyo alipokea ujumbe ''wa kwenda kuhiji Afrika'' wakati ambapo alitarajiwa kutia saini mkataba mpya katika klabu ya Everton.
''Alikuwa na uchawi na akapokea ujumbe aliotaka kwenda Chelsea'', alisema Moshiri.
Mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea walikuwa wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili Lukaku lakini badala yake akajiunga na Manchester United.
Mwezi Machi ajenti wa Lukaku Mino Raiola alikuwa amedai kwamba mkataba mpya wa kusalia Everton ulikuwa umekamilika asilimia 99.9.
''Tulimpatia kandarasi nzuri zaidi ya Chelsea na ajenti wake aliwasili kuja kutia kandarasi'' , Moshiri aliambia mkutano wa kila mwaka wa Everton.
Bilionea huyo wa Iran, Moshiri ambaye alikwa amewekeza dola milioni 150 katika deni la klabu hiyo, alisema kuwa Everton ilimpatia mshambuliaji huyo fedha nyingi ili kusalia.
''Swala la Lukaku halikuwa la kifedha. Iwapo nitaendelea kuwa miliki mkuu wa klabu hiyo maswala ya kifedha hayatakuwa tatizo''.Moshiri alisema kuwa Lukaku baadaye alimpigia simu mamake kabla ya mchezaji huyo kufichua kwamba alipokea ujumbe uliomwambia ajiunge na Chelsea
Maoni