Ruka hadi kwenye maudhui makuu

REAL MADRID KUVUNJA BENKI KUKAMILISHA UHAMISHO WA PAUL POGBA UTAVUNJA REKODI YA DUNIA

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.07.2019: Lindelof, Pogba, Bruce, Delph, Lukaku, Diaz, Kean



Barcelona inamnyatia beki wa Manchester United na raia wa Sweden Victor Lindelof, 24, huku ikiwa beki wa Ajax Matthijs de Ligt anatarajiwa kujiunga na Juventus. (Mundo Deportivo - in Spanish)


Real Madrid watalazimika kulipa dau litakalovunja rekodi la Ā£162m kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kutoka Manchester United. (Marca)

Mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Steve Bruce ataunga mkono ofa yoyote kutoka Newcastle baada ya kupigiwa upatu kumrithi Rafael Benitez. (Chronicle)


Naibu mkufunzi wa klabu ya Manchester City Mikel Arteta na mkufunzi wa Nice Patrick Vieira wameonywa kuhusu kazi ya Newvcastle na Benitez. (Sun)

Everton ni miongoni mwa klabu zilizo na hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Fabian Delph, 29. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutokubali uhamisho wa kuelekea Inter Milan na badala yake kusalia katika uwanja wa Old Trafford next season. (Sun)

Arsenal wamepatiwa ofa ya kumsaini mshambuliaji wa Real Madrid na raia wa Dominican Republic Mariano Diaz, 25, kwa dau la chini la Ā£18m. (Star)

Everton ina hamu ya kumsaini mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 19- wa Itali Moise Kean, ambaye klabu yake ya Juventus inataka dau la Ā£31m na kifungu cha kumnunua tena katika makubaliano yoyote. (Mail)

Fenerbahce inataka kumsaini mchezaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30 Mesut Ozil kwa mkopo kutoka Arsenal. (Sky Sports)

Manchester United imewasiliana na Southampton kutaka kujua kuhusu uwepo wa kiungo wa kati wa Gabon mwenye umri wa miaka 25 Mario Lemina. (Sky Sports)

Bournemouth wamempatia kandarasi mpya ya miaka mitano mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson huku West Ham, Chelsea na Everton zikihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27(Sun)

Liverpool wana matumaini kwamba mshambuyliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 24, atatia saini ya kandarasi mpya Anfield. (ESPN)

Crystal Palace inakaribia kumsaini kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Swansea na Ghana Jordan Ayew, 27, ambaye alihudumu msimu uliopita akiwa kwa mkopo. (Sky Sports)

Mpango a West Ham kumsaini mshambuliaji wa Celta Vigo Maxi Gomez umefutiliwa mbali baada ya klabu hiyo kufeli kukubaliana kuhusu mpango wa malipo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uruguay.. (Sky Sports)


The Hammers wamepatiwa ofa ya mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli, 28, kwa uhamisho wa bila malipo kama mbadala wa Wilson na Gomez. (Mirror)

Barcelona wana hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Romania Ianis Hagi, mwanawe mchezaji wa zamani wa Barcelona Georghe Hagi, kutoka klabu ya Viitorul Constanta na kumtoa kwa mkopo kwa klabu ya Real Valladolid. (AS - in Spanish

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...