SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa;
TANESCO imeanza utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa kwa Jengo la Ofisi za TANESCO Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam.
Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa , pia baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika Ofisi nyingine za TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama zaidi.
Uongozi wa Shirika pamoja na Wakala wa Majengo (TBA) wanaendelea kufanya taratibu zitakazo wezesha zoezi la ubomoaji wa Jengo kufanyika bila kuathiri huduma kwa Wateja wa Shirika.
Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais. Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Huduma za Umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya manunuzi ya LUKU.
Uongozi wa Shirika utaendelea kutoa taarifa kwa kadri zoezi hili linavyo endelea,
TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’
Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
www.twitter.com/tanescoyetu
Imetolewa Na: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO- MAKAO MAKUU.
Novemba 27, 2017
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni