Chama cha Zanu-PF kimemfuta Mugabe kama kiongozi wake Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama kiongozi wake.
Chama cha Zanu-PF kimemfuta Mugabe kama kiongozi wake
Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama kiongozi wake.
Kimemtua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.
Kufutwa kwa Bw. Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe 93, kumteua mke wake Grace kama makam wa rais.
Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe.
Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.
Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.
Maoni