Balozi wa Angola, Tanzania amtaka Eduardo dos Santos kushtakiwa
Balozi wa Angola nchini Tanzania amemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santos kushtakiwa kwa madai ya uhalifu aliyotekeleza wakati wa utawala wake wa miaka 38.
Ambrosio Lukoki amesema kuwa bwana dos Santos anafaa kujiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha MPLA kwa kuwa alikuwa anatumia wadhfa wake huo kuzuia kushtakiwa.
Rais mpya wa Angola Joao Lourenco hivi majuzi aliwafuta kazi wakuu wa polisi na vitengo vya ujasusi ,hatua iliokiuka sheria kwamba hatofanya hivyo kwa kipindi cha miaka minane.
Pia alimfuta kazi mwanawe bwana Dos Santos ambaye ni bilionea kama mkuu wa kampuni ya mafuta ya taifa hilo.
Bwana Lourenco kwa jina la utani JLo alichaguliwa na bwana Santos kusimama katika uchaguzi wa mwezi Agosti na wakati huo wachaganuzi walidhani kwamba ataendeleza uongozi wa bwana Santos
Maoni