Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameteliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania
Kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona Luis Enrique ametia saini mkataba wa miaka miwili kuchukua hatamu za kuifunza timu ya taifa ya Uhispania. Anachukua nafasi ya Julen lopetegui, ambaye alifutwa kazi katika mkesha wa kuanza kwa fainali za kombe la dunia baada ya kukubali kazi katika timu ya Real Madrid.
Fernando Hierro alichukua udhibiti wa timu hiyo kwa muda kwa ajili ya fainali hizo, ambapo mabingwa hao wa mwaka 2010 wa kombe la dunia waliondolewa katika awamu ya mtoano na wenyeji Urusi
Maoni