Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.
KILINGENI
Vatican NEWS Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.
Ask.Caccia:Hakikisha mazingatio ya maadili ya AI yawe msingi na usambazaji wa maendeleo
Vatican inasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba maendeleo na matumizi ya AI daima yanabaki katika huduma ya wanaume na wanawake,kukuza udugu na kuhifadhi fikra makini na uwezo wa utambuzi.Haya yameo katika hotuba ya Askofu Mkuu Caccia,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa huko New York,Marekani aliyotoa kwenye kikao maalum cha ECOSOC kuhusu Akili Mnemba jijini New York -Marekani tarehe 6 Mei 2025.
Na Angela Rwezaula -Vatican.
Askofu Mkuu Gabriele Caccia Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa alitoa hotuba yake katika Mkutano Maalum wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) ambalo ni jukwaa kuu la Umoja wa Mataifa, kuhusu Akili Mnemba tarehe 6 Mei 2025 huko mjini New York, Marekani. Katika Hotuba ya kikao cha kwanza kilichoongozwa na mada ya “Mitindo inayoibuka ya uvumbuzi wa Akili mnema AI na Maendeleo endelevu SDGs.” Swali elekezi lilikuwa: Je, watunga sera, viongozi wa sekta binafsi, wasomi na mashirika ya kiraia wanawezaje kufanya kazi pamoja ili kusawazisha udhibiti na uvumbuzi wa AI, kuhakikisha kwamba mazingatio ya kimaadili yanasalia katika msingi wa maendeleo na usambazaji wa AI?
Akili Mnemba kuunda udhibiti
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Caccia katika hotuba yake kuhusu mada hiyo alisema “ujumbe wake unakaribisha kuitishwa kwa mkutano huu maalum na alipenda kushiriki baadhi ya mawazo kuhusu jinsi ya kuhakikisha kwamba mazingatio ya kimaadili yanasalia kuwa msingi muhimu na usambazaji wa maendeleo ya AI.” Kwa njia hiyo “Akili Mnemba ni mafanikio ya ajabu ya kiteknolojia ambayo pia huleta hatari nyingi. Kwa sababu hii, jumuiya ya kimataifa ina wajibu muhimu wa kudhibiti matumizi ya AI katika aina zake nyingi. Ili kuunda udhibiti kama huo, ni muhimu kuuweka kwenye kanuni za kawaida za kimaadili ambazo zinaweza pia kuongoza miundo ya utawala, kama vile Mazungumzo ya Kimataifa kuhusu AI na Jopo Huru la Kisayansi la Kimataifa.
Sera zenye kujenga za AI zinahitaji ubunifu
Askofu Mkuu Caccia alisisitiza kuwa “Hakika, sera yenye afya kuhusu AI inahitaji ubunifu wa kiteknolojia kuwekwa ndani ya mradi mkubwa wa kutafuta manufaa ya wote. Kwa mantiki hii, Vatican inasisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha kwamba maendeleo na matumizi ya AI daima yanabaki katika huduma ya wanaume na wanawake, kukuza udugu na kuhifadhi fikra makini na uwezo wa utambuzi.”
Upamoja katika kufafanua maadili msingi wa mifumo ya kidhiti
Wito wa Roma kwa Maadili, uliotolewa mwaka wa 2020 na Chuo cha Kipapa cha Maisha, unaainisha kanuni kadhaa za kimsingi za kimaadili kama vile uwazi, ushirikishwaji, uwajibikaji, kutopendelea, kutegemewa na faragha. Mpango huu umewaleta pamoja watia saini wengi zikiwemo Serikali, Mashirika ya Kimataifa, taasisi nyingine na sekta binafsi, na umeidhinishwa na wengine wengi. Ni mfano halisi wa washikadau kuwa pamoja ili kufafanua msingi wa kimaadili ambao utakuwa muhimu kwa mifumo ya udhibiti ya siku zijazo na kuwasaidia wabunge katika juhudi zao za kusawazisha AI. uvumbuzi na udhibiti, huku tukitafuta “kukuza uwajibikaji na matumizi ya kimaadili ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi,” kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Baadaye, ambao Mkataba wa Kimataifa wa kidijitali ni kiambatisho
Maoni