Uchaguzi wa Papa,kutoka kwa moshi mweupe hadi Habemus Papam”



2025.05.08 Papa mpya 2025.05.08 Papa mpya   (@Vatican Media)

Hiki ndicho kilichotokea katika Kikanisa cha Sistine dakika chache ambazo zilifuatiwa na moshi mweupe,ambao unatokea kabla ya tangazo kuu la Kardinali shemasi Mamberti,akiwa katikati ya Dirisha la Baraka la Basilika ya Mtakatifu Petro kwa jina jipya la Askofu wa Roma.

Na Alessandro Di Bussolo na Angella Rwezaula – Vatican.

Moshi mweupe ulitokea katika bomba lililounganishwa katika Kikanisa cha Sistine, ambao umeashiria kutangaziwa waamini na ulimwengu mzima kuwa amechaguliwa Askofu mpya wa Roma, mfuasi wa Petro. Lakini je ni kitu gani kilitokea chini ya picha za msanii Michelangelo, dakika chache kabla, na ni kitu gani kitaendelea hadi kutangazwa kwa jina jipya la Papa, litakalotangazwa baada ya neno la: "Habemus Papam” yaani "Tunaye Papa" kupitia katikati ya dirisha la Baraka la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na Kardinali, Shemasi wa ufaransa, Dominique Mamberti? Jina linalosubiriwa kwa hamu kubwa.

Moshi mweupe   (@Vatican Media)

Ibada ya kukubaliwa

Kwa misingi iliyowekwa na kanuni ya Ordo rituum Conclavis (Kitabu cha ibada ya mkutano Mkuu wa uchaguzi (Ordo Rituum Conclavis,ambacho kiliidhinishwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili mwaka 1998, lakini hakikutolewa hadi baada ya kifo chake mwaka wa 2005 na ya Katiba ya  Kitume ya Kanisa katolki ya Universi Dominici Gregis,iliyotolewa na Papa Yohane Paulo wa Pili tarehe 22 Februari 1996.) Kardinali aliyepo katika Kikanisa cha Sistina alifikia kura zinazohitajika na uchaguzi umefanyika kikatiba. Kardinali wa kwanza kwa mpangilio na mzee au yeye aliyechaguliwa kwa mjibu huo kwa niaba ya Baraza la Makardinali wateule aliuliza kwa lugha ya kilatini kukubaliwa kwa aliyechaguliwa kwa maneno yafuatayo: “Unakubali uchaguzi wako kikatiba kuwa Baba Mtakatifu.” Na baada ya kukubali, alimuuliza tena swali: “Je unataka kuitwa nani?” kwa njia hiyo Mshereheshaji wa Liturujia za Kipapa kwa kazi yake, kutia saini na kwa kuwa na mashuhuda wawili wa maadhimisho, waliandika hati ambayo inabainisha kukubali kwa Baba Mtakatifu mpya na jina ambalo yeye amechagua.

Waamini katika Uwanja

Hitimisho la Mkutano Mkuu

Katika mkutano mkuu wa uchaguzi kwa usahihi, Katiba ya kitume ya Universi Dominici Gregis, inahitimisha hivyo baada ya Papa mpya “kukubali uchaguzi wake, labda kama Yeye anajibu kinyume chake.” Kwa hiyo wanaweza kuingia katika Kikanisa cha Sistine Katibu Msaidizi wa Vatican, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Mataifa, na mwingine ambaye lazima ashughulike na Papa mteule juu ya mambo ambayo ni muhimu kwa wakati huo.

Moshi na “Chumba cha Machozi

Baada ya kumaliza hatua ya kukubali, kadi zote za uchaguzi zinachomwa na maandishi mengine yaliyotumika kwa ajili ya uchaguzi na moshi mweupe umeonesha kwamba amechaguliwa Papa mpya. Wakati waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakishangilia na ulimwengu ukibaki na shauku ya kujua jina jipya la Papa, aliyechaguliwa, anatoka katika Kikanisa cha Sistina na kuingia katika Skrestia, kwa kile kiitwacho: “chumba cha machozi.” Hapo kwa msaada wa Mshereheshaji wa Liturujia za kipapa, anavua nguo za ukardinali na kusaidiwa kuvaa mavazi kati ya matatu yaliyo tayarishwa tayari kwa vipimo tofauti na kujikita katika sala za kwa dakiki chache.

Sherehe za kwanza(0ssequio)heshima na utii na(Te Deum)sala ya shukrani

Baada ya kurudi tena katika Kikanisa cha Sistine Papa aliyechaguliwa kuongoza kiti kikuu na ambapo muda mfupi kutakuwa na maadhimisho mafupi kwa salamu kutoka kwa Makardinali wa kwanza kwa daraja la Maaskofu. Kardinali wa kwanza kwa Makuhani anasoma kifungu cha Injili ambacho kinaweza kuwa: “Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa lako” au “Chunga Kondoo wangu.” Na hatimaye Kardinali Shemasi atasali sala kwa Mfuasi wa Petro ambaye amechaguliwa. Na kufuatia na Makardinali wote waliopiga kura waliopo kwa mujibu wa kanuni husika wanajiweka katika mstari mbele ya Papa Mpya ili kuonyesha heshima na utii wao. Kwa hiyo wote pamoja wanaimba Wimbo wa Shukrani  kwa Mungu:“Te Deum”, ambao unanzisha na Papa aliyechaguliwa.

Sala ya Papa mpya katika Kikanisa cha Pauline

Kardinali shemasi Dominique Mamberti anafikia katikati ya dirisha la Baraka na kutangaza kwa watu uchaguzi na jina la Papa mpya kwa mtindo huu“Annuntio vobis gaudium magnum: habemus Papam!" yaani: “Tangazo la furaha kwenu. Ninawatangazia kwamba tunaye Papa mpya.” Na wakati huo huo, Papa aliyechaguliwa, anatoka katika Kikanisa cha Sistine ili kuja katikati ya dirisha la Baraka, anapitia katika kikanisa cha Pauline, mahali ambapo anatulia kidogo kusali, kwa kimya mbele ya Sakrameti Takatifu na baadaye anaendelea na safari hadi katikati ya dirisha la Kanisa kuu, mahali ambapo anatoa salamu yake na kutoa baraka ya kwanza ya kitume ya “Urbi et Orbi”:  ya mji wa Roma na Ulimwengu mzima.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU