Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwanamke aliye na ushawishi mkubwa Korea Kaskazini atahudhuria michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itakayozinduliwa Pyeongchang ,siku ya Ijumaa, mawaziri jijini Seoul wanasema.
Kim Yo-jong, atakuwa ndugu wa kwanza wa karibu katika familia ya Kim atakayevuka mpaka.
Korea zote mbili zitaandamana pamoja chini ya bendera moja katika sherehe za uzinduzi.
Ushiriki wa Korea Kaskazini umeonekana kama kulegeza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo, Marekani na Japan wameishtumu Korea Kaskazini kwa kutumia michezo hio kama chama cha propaganda.
Kim Yo-jong ni nani?
Akiaminiwa kuzaliwa mwaka 1987, ni mtoto wa kike wa mwisho wa hayati kiongozi Kim Jong-il na ni dada yake wa tumbo moja Kim Jong-un. Anazidiwa umri na kaka yake kwa miaka minne na inasemekana kwamba wana uhusiano wa karibu sana.
Anasemekana kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala.
Kim Yo-jong akiwa kwenye sherehe ya kuzindua jengo la gorofa la makazi Pyongyang 2017
Kim Yo-jong amekuwa akionekana sana miaka ya hivi karibuni, ikiwa kazi yake kuu ni kulinda muonekano wa kaka yake kupita cheo chake kwenye idara ya propaganda ya chama.
Familia yenye usiri zaidi Korea Kaskazini
Maoni