Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine


Seneta Rand Paul katikati akiwa na marafikize kutoka kwa bunge la uwakilishi muda mfupi baada ya bunge la seneti kuitisha mapumziko

Huduma za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa.


Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika.


Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi.


Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu.



Hatahivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini.


Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili.



Maboksi ya pizza yalipelekwa katika bunge hilo huku watu wakitarajia kwamba utakuwa usiku mrefu kwa viongozi hao

Mkwamo huo ulitarajiwa ikiwa imesalia saa moja kabla ya muda kukamilika wakati bunge la seneti lilipopiga kura ya mapumziko.


Lakini licha ya kuchleweshwa ,bunge hilo linatarajiwa kupigia kura matumizi hayo.


Bunge la uwakilishi halitapiga kura yoyote hadi pale bunge la seneti litakapoidhinisha matumizi hayo.


Haijulikani ni vipi bunge la Congress litaendelea na vile huduma za umma zitakavyoathirika.


Hatua hiyo itasababisha kupanda kwa matumizi hadi $300bn (£215bn) - Kitu ambacho seneta Paul anasisitiza hawezi kuunga mkono.



Matumizi ya bajeti ya serikali ya Marekani

Huku ufadhili wa bajeti ya idara ya ulinzi ukionekana kuwafurahisha maafisa wa maswala ya usalama, wahafidhana wanapinga athari za deni la taifa hilo.


Seneta Paul aliyekasirika aliwakemea wenzake wa chama cha Republican akidai ufisadi unaoendelea.


''Niligombea wadhfa huu kwa sababu nilikuwa mkosoaji mkubwa wa deni la Trilioni za madola katika utawala wa rais Obama


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...