Kenya yatetea uamuzi wa kumfukuza Miguna

Bwana Miguna Miguna na Raila Odinga

Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake


Jana usiku mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana Miguna


Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009.


"Kwa mantiki hiyo hati ya kusafiria ya Kenya ya bwana Miguna ilikuwa na bado ni batili", alifafanua bwana Njoka


Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baada ya kushiriki katika kiapo kisicho rasmi cha Raila Odinga kuwa rais wa watu wa Kenya mwezi uliopita.


 Bwana Raila Odinga akiapishwa uraisi wa watu

Odinga ni mwanasiasa wa upinzani ambaye alisusia marudio ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika mwaka jana, kwa madai kuwa haukuwa huru na wa haki


Rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi kwa kura nyingi katika uchaguzi huo


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU