Waandana nje ya ubalozi wa Rwanda
Mamia ya waandamanaji wamekusanyika nje ya ubalozi wa Rwanda nchini Israel katika mji wa Herzeliya kulalamikia sheria mpya ya wahamiaji nchini humo.
Wengine wakiwa wamebeba mabango yanayosema "nitafukuzwa mpaka nife kwa sababu mimi ni mweusi"kutokana na mapendekezo ya kuwa wahamiaji kutoka Afrika hawakaribishwi nchini Israel kuliko wahamiaji kutoka bara la ulaya kwa sababu ya ubaguzi wa rangi.
Waandamanaji wa Afrika nchini Israel
Wahamiaji wengi wa Afrika nchini Israel wanatoka Eritrea na Sudan Kusini
Maandamano hayo nje ya ubalozi wa Rwanda yalikuwa yanamtaka Rais Paul Kagame ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na rais wa Rwanda kupinga mpango wa Israel wa kuwaondoa wahamiaji 38,000 ambao wengi wao ni kutoka Eritrea na wenye asili ya Sudan Kusini.
Mwanzoni mwa mwaka ,serikali ya Israel ilitoa taarifa kwa maelfu ya wahamiaji wa Afrika kuondoka nchini humo au watakabiliana na kifungo.
Inasemwa kuwa wahamiaji watapewa dola 3500 za kimarekani ili waondoke ndani ya siku 90,na wamepewa uchaguzi wa aidha kurudi katika nchi walizotoka au kwenda katika nchi yoyote inayoendelea.
Na wasipoondoka ,mamlaka ya Israel yametishia kuwa wataanza kuwafunga kuanzia mwezi april
Maoni