KWANINI RUBANI WA NDEGE ZA KIVITA AKIOKOKA KWENYE AJALI YA NDEGE HAWEZI TENA KURUSHA NDEGE


Tangu mwishoni mwa miaka ya 1940, maelfu ya marubani wa kivita wamenusurika kwenye ajali mbaya kutokana na matumizi ya viti vya kisasa vya kutoroka nje ya ndege "Ejection Seat"


Kutoroka huko kunahusisha kuuweka mwili wa binadamu katika nguvu za uvutano (G-Force) zinazofikia 12-14 Gs ndani ya sekunde, na kusababisha mkandamizo wa uti wa mgongo, kuvunjika pingili, au uharibifu wa muda mrefu wa 'musculoskeletal'.

Kila utorokaji huja kwa gharama kubwa ya afya na kikazi, huku marubani wengi ambao hujifyatua nje zaidi ya mara moja hawarejei kwenye majukumu ya mstari wa mbele wa kuruka.

Kujifyatua au kutoroka nje ya ndege zoezi la vurugu kwa asili yake ya kimuundo, na hutumia chaji za vilipuzi au roketi kulipua kiti na rubani kurushwa nje ya ndege kwa sekunde.

Mkandamizo wa juu unaweza kufikia 20 Gs (Hii ni mara 20 ya uzito wa mwili wako) ambapo hukandamiza mgongo na kuumiza mwili.

Marubani mara nyingi hupata nyufa ya uti wa mgongo, majeraha ya shingo, au majeraha ya tishu laini.

Zaidi ya majeraha yanayoonekana, utorokaji huu unaweza kusababisha uharibifu uliofichwa, kama vile diski za mgongo kudhoofika au kuteleza kwa muda, maumivu ya muda mrefu ya mgongo, kupoteza ujasiri, au kupungua uwezo wa utendaji.

Vikosi vya anga vimeweka viwango na sheria kali madhubuti zankiafya kwa marubani wa kivita, lakini baada ya jeraha la mgongo linalohusiana na kufyatuka nje ya ndege, rubani huenda asifikie viwango hivi tena.

Viti vya kisasa vya kujifyatua huokoa maisha, lakini kwa malipo ya afya ya rubani.

Utorokaji mmoja unaweza kuwa hauna madhara sana, lakini mara mbili au zaidi huacha majeraha ambayo yanashindwa kusalia kwenye viwango vya matibabu vya anga.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU