RC ARUSHA AONYA WAKANDARASI WABABAISHAJI
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo ameonya Wakandarasi wanaofanya ubabaishaji kwenye miradi ya barabara za vijijini Mkoani Arusha kwa kutopewa tenda za serikali na badala yake wachukuliwe hatua za kisheria.
Gambo ametangaza marufuku kwa wakandarasi wababaishaji kupewa kandarasi wakati akikabidhi mikataba ya kwa
wakandarasi wa wilaya za saba za mkoa wa Arusha ikiwemo Arusha,Meru na Karatu .
Aidha amewataka Wakandarasi kuhakikisha kuwa wanakamilisha miradi kwa wakati na kutumia vizuri fedha za walipa kodi na kuepuka kutekeleza miradi chini ya kiwango.
Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Richard Kwitega amesema kuwa serikali imewapa kipaumbele Wakandarasi wazawa ili waweze kuleta tija kwenye miradi ya Barabara ambazo zitachochea maendeleo ya wananchi.
Kaimu Mratibu wa Tarura mkoa wa Arusha Dickson Kanyankole amesema kuwa miradi hiyo itatekelezwa katika wilaya 7 na ambayo imegharimu fedha nyingi ambapo mikataba 36 imesainiwa yenye thamani ya shilingi bilioni 6.
Wakandarasi Patrick Swai na Jeremiah Ayo wamesema kuwa watafanya kazi kwa weledi na kuepuka vitendo vya rushwa amabavyo vimekua vikichangia kuzotesha maendeleo ya miradi mingi.
Patrick ameishukuru serikali kwa kuwaondolea kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika miradi wanayotekeleza jambo ambalo linawapunguzia mzigo wa kodi na kuwawezesha kufanya kazi vyema
Maoni