Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Miito yaongezeka kumtaka Mugabe kuachia ngazi, Zimbabwe


Raia nchini Zimbabwe wameanza kuangazia mustakabali wa taifa hilo bila ya kiongozi wao aliyekaa madarakani kwa takriban miongo minne, wakati mazungumzo ya maridhiano yakiendelea.
Raia nchini Zimbabwe wameanza kuangazia mustakabali wa taifa hilo bila ya kiongozi wao aliyekaa madarakani kwa takriban miongo minne. Jeshi limechukua nafasi ya rais Robert Mugabe mwenye miaka 93, shujaa wa ukombozi aliyegeuka kuwa mtawala wa kiimla, ambaye kwa sasa yuko katika kizuizi cha nyumbani. zaidi kuhusu kinachojiri Zimbabwe.
Taifa hilo liliachwa na mshangao baada ya rais huyo mkongwe kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani jioni ya Jumanne, na wanajeshi kuweka doria kwenye maeneo muhimu katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, na maafisa wake waandamizi kutangaza kuchukua udhibiti wa kituo cha televisheni.
Kiongozi wa upinzani aliyerejea nchini humo, Morgan Tsvangira amesema ni lazima rais Robert Mugabe ajiuzulu. Ametaka serikali ya mpito kujadiliwa, na kuhusisha pande zote pamoja na kufanywa mageuzi mapana kabla ya uchaguzi mkuu.
Tsvangirai amewaeleza waandishi wa habari mjini Harare kwamba kunatakiwa kuwepo na mkakati wa baada ya kufanyika kwa uchaguzi ili kuhakikisha utulivu, na mkakati huo usimamiwe na jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC na Umoja wa Afrika, AU.
Makamu wa rais aliyefutwa kazi mwaka 2014 Joice Mujuru kwa upande wake ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki, wakati mchakato wa kuundwa kwa serikali ya mpito ukiendelea na kuhusisha pande zote. Mujuru alifutwa kazi na rais Robert Mugabe kwa madai ya kupanga mikakati ya kuwania nafasi ya uraia.
Joice Mujuru, aliyewahi kuwa makamu wa rais wa Robert Mugabe ataka kuondolewa kwa upendeleo kwa raia nchini humo.
Makundi ya kiimani na haki za binadamu yataka utulivu.
Kwa upande mwingine, kampeni iliyonzishwa na mchungaji Evan Mawarire kupitia mtandao wa kijamii yenye hashtag #ThisFlag Movement imeibua maandamano makubwa yanayoipinga serikali ambayo hayajatokea katika kipindi cha muongo mmoja, na inataka raia kuhakikisha amani inasalia nchini humo.
Vyama vya upinzani, asasi za kiraia na makundi ya kiimani yametaka utulivu na kuheshimiwa kwa haki wakati mazungumzo yakiendelea ili kutatua mzozo uliopo na ambayo labda yatakayofikisha hatma ya utawala wa muda mrefu wa rais Robert Mugabe. Zaidi ya asasi 100 za kiraia yanataka Mugabe kuachia madaraka kwa amani.
Mawaziri kutoka mataifa wanachama wa Jumuiya ya uchumi kwa nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, chini ya uenyekiti wa Afrika Kusini na Angola, wanakutana leo hii nchini Botswana kujadili sintofahamu hiyo, na mapendekezo yao yatawasilishwa kwa wakuu wa nchi na serikali.
Ubalozi wa Marekani umewataka raia kujiepusha na mizunguko isiyo ya lazima, wakati ambapo hali nchini humo bado ni tete. Serikali ya Uingereza, yenyewe imewataka raia wake waliopo, Harare kujiepusha na mikusanyiko na maandamano yoyote.
Si Mugabe wala mkewe, Grace ambao wamezungumza chochote tangu kuanza kwa operesheni hiyo ya kijeshi. Lakini Wazimbabwe wengi wanataraji kwamba mzozo huo utafungua njia ya maisha bora zaidi huko mbele.
Msemaji wa chama tawala, ZANU-PF, Simon Khaya Moyo, amesisitiza kwamba hili ni suala la kawaida. Raia wamepuuzia uwepo wa wanajeshi kwenye mitaa ya mji wa Harare na kuendelea na shughuli zao, huku wachambuzi wakielezea kwamba kuna uwezekano kuwa Mugabe na jeshi wanajadiliana kuhusu serikali ya mpito.
Rais Mugabe, mkewe Grace na washirika waandamizi wa kisiasa wanazuiwa nyumbani, katika kasri la Mugabe maarufu "Blue House”, mjini Harare, kimesema chanzo kimoja cha kisiasa.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...