Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mchezaji wa bora wa Afrika taji la BBC mwaka 2017: Mpigie kura unayempenda

 Upigaji kura wa mchezaji atakayeshinda taji la mchezaji bora wa Afrika la BBC mwaka 2017 umeanza. Wachezaji watano walioorodheshwa ni Pierre-Emerick Aubameyang, Naby Keita, Sadio Mane, Victor Moses naMohamed Salah. Walitangazwa katika kipindi maalum cha moja kwa moja katika BBC. Waliowahi kushinda tuzo hiyo awali ni pamoja na nyota wawili wa Ivory Coast Didier Drogba na Yaya Toure, Jay-Jay Okocha wa Nigeria na jagina wa Liberia George Weah. Jopo ambalo liliwashirikisha miongoni mwa wengine Emmanuel Amuneke, mshindi wa ubingwa Afrika na Olimpiki 1996, Arnaud Djoum, mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 akiwa na Cameroon, na Jean Sseninde, kutoka Uganda anayechezea Crystal Palace Ladies, walikuwepo kujadili majina ya walioteuliwa kushindania tuzo hiyo. Watano hao watakuwa wakitumai kufuata nyayo za mshindi wa mwaka jana Riyad Mahrez, aliyeng'aa mwaka 2016 akichezea mabingwa wa Ligi ya Premia mwaka huo Leicester City na Algeria. Mashabiki wanaweza kupigia mchezaji wanayetaka ashinde kupitia ukurasa wa soka ya Afrika katika tovuti ya BBC, BBC African football, hadi upigaji kura utakapokamilika 18:00 GMT Jumatatu, 27 Novemba. Mshindi atatangazwa moja kwa moja 17:30 GMT Jumatatu, 11 Desemba. Piga kura hapa Pigia kura mshindi wa tuzo ya BBC kwa mchezaji bora Afrika 2017. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon naBorussia Dortmund  Aubameyang: Mchezaji hatari kwa ufungaji mabao Ujerumani Hakuna mara hata moja katika historia ndefu ya ligi kuu wa Ujerumani Bundesliga ambapo mchezaji kutoka Afrika alikuwa ameongoza kwa ufungaji wa mabao ligini peke yake hadi pale Pierre-Emerick Aubameyang alipofunga mabao 31 msimu wa 2016-17. Idadi yake ya mabao ilimuwezesha raia huyo wa Gabon kuvunja hata rekodi iliyowekwa na mchezaji wa Ghana Tony Yeboah, ambaye alimaliza akiwa anashikilia nafasi ya ufungaji mabao ligini na mchezaji mwingine miaka ya 1990. Aubameyang: Mwafrika anayevuma Ujerumani Kadhalika, ilikuwa ni mara ya nne kwa mchezaji kufunga Zaidi ya mabao 30 katika msimu mmoja Bundesliha - na mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40. Naby Keita - RB Leipzig na Guinea  Naby Keita: Mchezaji aliyewavutia sana Liverpool Naby Keita huenda alianza msimu wa 2016-17 kama mchezaji asiye na umaarufu nchini Ujerumani, lakini alikamilisha msimu huo jina lake likiwa katika kikosi cha timu ya mwaka - kura iliopigwa ambapo mchezaji huyo wa Guinea alipata kura nyingi kushinda kiungo wa kati yeyote yule. Klabu ya Red Bull Leipzig ndiyo iliowashangaza wengi katika msimu wa 2016-17, huku ikimaliza katika nafasi ya pili (na kufuzu katika mashindano ya vilabu bingwa), lakini ilikuwa kiungo huyo wa kati aliyeisadia timu hiyo kuwa katika nafasi ya pili. Dakika tano tu baada ya kuchezeshwa katika kikosi cha kuanza mechi mara ya kwanza katika Bundesliga, Keita aliyenunuliwa kutoka klabu dada cha Red Bull Salzburg ya Austria, alifunga bao la ushindi dhidi ya Borussia Dortmund kunako dakika ya 89 na hivyo basi kushinda taji la mchezaji bora na timu bora ya msimu. Kwa jumla, alifunga mabao manane, mojawapo likiwa bao lililoorodheshwa kuwania tuzo ya bao bora la msimu huku akitoa usaidizi katika ufungaji wa mabao 7. Naby Keita: Mchezaji aliye na matumaini makubwa Mchezaji huyo pia anapendwa sana kwa uwezo wake wa kurudi nyuma na kulinda lango. Sadio Mane -Senegal & Liverpool  AFOTY 2017: Wasifu wa Sadio Mane Nyota wa Senegal na Liverpool Sadio Mane alifanya vizuri sana mwaka 2017 hivi kwamba alipigiwa kura na wachezaji wenzake kuwa kwenye kikosi bora cha PFA. Kadhalika, alikuwa mmoja kati ya Waafrika wawili kuteuliwa kushindania tuzo ya Ballon d'Or. Pia alitekeleza wajibu mkubwa katika kuiongoza Senegal kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2002. Katika ufungaji wake bora zaidi akiichezea Senagal mwaka mmoja, Mane alifunga mabao manne katika mechi 9 za kimataifa. Ilikuwa ni tofauti sana na mwanzoni mwa mwaka kwani Mane alionesha ukakamavu wake kiasi cha kufikia kasi yake ya umeme, ujanja wake na ustadi wa kutia mabao kimiani. Baada ya kufunga katika mechi za kwanza mbili hatua ya makundi katika mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka wa Mane ulibadilika na kuwa mchungu. Mane: Mchezaji aliyewafaa sana Liverpool Alishindwa kufunga mkwaju wa penalti wakati wa mikwaju ya kuamua mshindi dhidi ya Cameroon na akawawezesha samba hao ambao baadaye waliibuka mabingwa kufika hatua ya nne bora. Hilo lilimdhoofisha sana Mane, machozi yakionekana kutiririka kama maji kwenye uso wake siku hiyo. Victor Moses -Nigeria na Chelsea  Victor Moses: Mchezaji aliyewavusha Nigeria hadi Urusi Victor Moses atakapotafakari kuhsuu maisha yake ya uchezaji, kuna uwezekano mkubwa kwamba kiungo huyo wa kati wa Nigeria na Chelsea atautazama msimu wa 2016-17 kama wakati ambao nyota ya jaha ilimuangazia. Baada ya miaka kadhaa ya kutanga jangwani akiwa anatumwa nje kwa mkopo mara kwa mara, mchezaji huyo wa miaka 26 hatimaye alitia guu na kutulia Stamford Bridge, sana kiasi kwamba alitekeleza mchango muhimu katika kikosi kilichoshinda Ligi ya Premia. Siku ambayo Moses ataikumbuka ni 1 Oktoba baada ya kocha wa Chelsea Antonio Conte baada ya vipigo vikali mfululizo kutoka kwa Arseanal na Liverpool alipobadili mfumo na kucheza 3-4-3 na kiungo huyu raia wa Nigeria akachezeshwa kwenye nafasi asiyoizoea pembezoni kwenye winga ya kulia kwenye mchezo dhidi ya Hull City. Ulikuwa mchezo wake wa kwanza ligi kwake kuanza kwenye kikosi akiichezea Chelsea kwa karibu miaka mitatu. Lakini Moses alikuwa mchezaji bora na aliichangamkia sana fursa hiyo na kuonyesha mchezo wake wa kushambulia na pia kuwa mkabaji hali ikilazimu. Moses hatimaye alitulia na kutamba Chelsea Ushindi dhidi ya Hull ulikuwa mwanzo wa ushindi mara 13 mfululizo kwa Chelsea kwenye ligi kuu nchini Uingereza na ukawa ni mchezo wa 22 wa Moses kuanza kwenye kikosi ligini mtawalia, hadi alipotupwa nje na jeraha kwa muda mwezi Aprili. Mohamed Salah -Egypt & Liverpool  AFOTY 2017: Safari ya Salah kufikia ufanisi Mohamed Salah huenda amefunga mabao chungu nzima lakini atakumbukwa nchini Misri kwa kitu kimoja- bao la dakika za lala salama dhidi ya Congo mwezi Oktoba. Bao hilo liliwawezesha Mafirauni kufuzu kwa mara ya kwanza kwa michuano ya Kombe la Dunia baada ya kipindi cha robo karne. Misri walifanikiwa kuwa mabingwa wa Afrika mara saba lakini walikuwa hawajawahi kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia tangu 1990, na ikiwa katika dakika za lala salama walishinda penalti huku ikiwa matokeo ni 1-1 hatua iliyozua hisia zisizokuwa za kawaida nje na hata ndani ya uwanja. Na mchezaji huyo ambaye alikuwa ametulia na kutobabaishwa alifunga bao hilo lililowafurahisha mashabiki wengi wa nyumbani na kumlazimu Rais Abdul Fattah Al Sisi kumpongeza kwa kuweza kuhimili shinikizo za raia milioni 80 wa Misri. Bao hilo lilimpatia umaarufu wa kuwa mfalme wa Mafirauni 2017, huku timu hiyo ikipewa jina la utani ''Misri ya Salah'' kutokana mchezo wa kasi wa mshambuliaji huyo ambaye aliiwezesha Misri kuwika. Salah: Mchezaji aliyesaidia kuwafikisha Misri Kombe la Dunia Kwa mfano Salah alifunga mabao matano kati ya mabao saba yaliyofungwa wakati timu hiyo ikitafuta kufuzu kwa Kombe la Dunia la Urusi


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...