Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United katika mechi ya Jumamosi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford
Zlatan Ibrahimovic na Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United katika mechi ya Jumamosi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford.
Mshambuliaji Ibrahimovic , 36, bado hajashirikishwa katika mechi yoyote msimu huu baada ya kupata jeraha la goti mnamo mwezi Aprili.
Kiungo wa kati Paul Pogba , 24, hajaichezea timu yake tangu alipopata jeraha la nyuma ya goti dhidi ya klabu ya Basel mnamo mwezi Septemba.
Beki Marcos Rojo pia anapatikana na mkufunzi Jose Mourinho alisema kuwa wote wataorodheshwa.
''Paul unaweza kuona. Unaweza kugundua kwamba kulikuwa na Manchester United msimu huu kabla na hata baada ya jeraha lake'', aliongezea Mourinho.
''Ana uwezo ambao hubadilisha vile tutakavyocheza mechi zetu''.
Mshambuliaji wa zamani wa Sweden Ibrahimovic ameichezea klabu hiyo mechi 46 na kufunga magoli 28 msimu uliopita.
Aliachiliwa na klabu hiyo mnamo mwezi Juni baada ya msimu wake kumalizwa na jereha la nyuma ya goti lakini akapewa mkataba mwengine mpya wa mwaka mmoja mnamo mwezi Agosti.
''Msimu uliopita tulimchezesha Zlatan kila dakika'', aliongezea Mourinho.
''Tulijifunza kucheza bila yeye.Lakini tunamkaribisha ni mchezaji mzuri sana''.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni