Trump ametishia kulipiza kisasi kwa sababu ya ''upumbavu'' Macron
Raisi wa Marekani Donald Trump amemshutumu raisi wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa ''upumbavu'' kuhusu kodi ya huduma za kidigitali, na kudokeza kuwa atalipiza kisasi kwa kutoza kodi mvinyo wa Ufaransa.
Trump alionyesha ghadhabu yake kwenye ukurasa wa Twitter siku ya Ijumaa, akijibu mipango ya Ufaransa kutoza kodi mashirika kama Google.
Mamlaka za Ufaransa zimedai kuwa makampuni hayo hulipa kiasi kidogo au kutolipa kabisa katika nchi ambazo si makao yao makuu.
Utawala wa Trump umesema kodi hiyo inawalenga makampuni makubwa ya teknolojia ya Marekani isivyo haki.
''Ufaransa inampango wa kutoza kodi makampuni yetu makubwa ya teknolojia. Yeyote anayepaswa kuyatoza kodi ni nchi makampuni yanakotoka, yaani Marekani'', Trump aliandika kwenye ukurasa wa Twitter.
''Tutatangaza hatua za kulipiza kisasi kutokana na upumbavu wa Macron muda mfupi ujao.Siku zote nimesema mvinyo wa Marekani ni bora kuliko wa Ufaransa!''
Simulizi ya kushangaza ya wahamiaji wa jadi Marekani
Marekani ni mtumiaji mkubwa wa mvinyo duniani na ni soko kubwa kwa bidhaa hiyo, huku Ufaransa ikiwa miongoni mwa nchi zinazoingiza zaidi mvinyo wake nchini Marekani.
Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire alijibu siku ya Ijumaa kwa kusema kuwa Ufaransa itabaki na msimamo wake wa mipango ya kutoza kodi makampuni ya teknolojia.'' Dunia nzima inakabiliwa na changamoto ya masuala ya kodi kwa makampuni yanayotoa huduma za kidigitali,''alisema.
Raisi Macron na raisi Trump mapema siku ya Ijumaa walijadili kuhusu uhitaji wa makubaliano ya pamoja ya kimataifa kuhusu kutoza kodi makampuni ya teknolojia, Ofisi ya raisi wa Ufaransa imeeleza.
Serikali ya Ufaransa imedai kuwa makampuni kama Apple, ambayo makao makuu yake ni nje ya Ufaransa, hulipa kidogo au kutolipa kabisa kodi inayotokana na mauzo yao nchini Ufaransa.
Mpango wa kodi ulipitishwa na Bunge la Ufaransa siku ya Alhamisi, juma moja baada ya kupitishwa kwenye bunge dogo la nchi hiyo.
Kampuni yoyote ya kidigitali yenye mapato zaidi ya pauni milioni 670 ambapo takribani Euro milioni 25 iwe imepatikana nchini Ufaransa- itapaswa kulipa kodi.
Siku ya Ijumaa, raisi Trump alitahadharisha kampuni ya Apple kuwa haitapata unafuu wa kodi ya vifaa vinavyotengenezwa China. ''Tengenezeni nchini Marekani, hakuna kodi!'' aliandika.
Ufaransa imesema nini?
Akitetea kodi mpya siku ya Alhamisi, bwana Le Maire amesema Ufaransa ''ni taifa huru na linajiamulia lenyewe kuhusu sheria za kodi''.
Takribani makampuni 30 watalipa kodi- hasa ya Marekani kama vile Alphabet, Apple,Facebook, Amazon na Microsoft, makampuni ya China, Ujerumani, Uhispania na Uingereza pia yataathirika, halikadhalika kampuni ya matangazo mtandaoni ya nchini humo, Criteo
Maoni
› › Learn How To Play › › Learn Learn septcasino How To Play A Baccarat Strategy Guide 1xbet korean and How to Win Tips and Rules worrione for Beginners. Learn More.