MTEULE THE BEST
Waziri wa utalii nchini
Brazil,Henrique Alves amejiuzulu siku moja baada ya kushutumiwa
kujihusisha katika kampeni zisizo halali za kujipatia fedha kutoka kwa
wanyonyaji wakubwa wa rushwa wa taifa wa kampuni ya mafuta, Petrobras.
Alves ni waziri wa tatu kujiuzulu katika wa utawala wa raisi Michel
Temer ambaye yuko katika muhula wa serikali iliyojaa kashfa.
Waziri Alves akiwa bado anazipinga tuhuma hizo.Jumatano ,mahakama kuu imetoa ushaidi kutoka kwa mmoja wa wakuu wa Pretrobas, Sergio Machado ambaye amewahusisha wanasiasa ishirini wenye majina makubwa akiwemo raisi Temer ambaye pia amepinga kuhusika kuwasaidia wanachama wa chama chake katika harakati hizo zisizo halali.
Maoni