Huwenda nyakati zikawalazimu Diamond Platnumz na Alikiba kuwa kitu kimoja kwenye muziki kwa sasa. Ni kipindi kirefu wameripotiwa kutoelewa ingawa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hilo.
Kwa sasa Diamond yupo katika pilika pilika za kuhakikisha tamasha lake la Wasafi Festival linafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wakati akieleza kuhusu ujio wa Wasafi Festival alieleza kuwa angetamani na Alikiba angekuwepo kitu ambacho kiliibua mjadala mpana zaidi.
Alikiba tayari amekubaliwa kuwa sehemu ya udhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Wengi wamesema huu ni mwanzo nzuri kwa wasanii hawa kurudisha ushirikiano wao na kufanya vitu vikubwa zaidi.
Kwanini Studio
Hapo jana Diamond Platnumz akiwahojiwa na kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya alisema si Alikiba kushiriki Wasafi Festival tu bali hata kufanya wimbo pamoja yupo tayari.
"sio tu Alikiba mtu yeyote ambaye anahisi kuna sehemu nikimuweka Diamond itanisaidia katika kazi yangu asisite kunitafuata kwa sababu mwisho wa siku hii ni biashara, usimchukulie mtu personal na kuifanya iwe tatizo," amesema Diamond.
Je Itawezekana ?
Bila shaka inaikumbua project ya Kigoma All Stars ambayo ilikuja na ngoma yao inayokwenda kwa jina la Leka Dutigite ambayo ilifanya vizuri kwa kiasi kibwa.
Kigoma All Stars ilikuwa na wasanii kama Abdu kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond plantimuz, kigoma all stars, Leka Dutigite, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy dimpoz, Queen Darling, Rachel na Alikiba.
Wimbo wao wa pili baada ya Leka Dutigite ilifahamika kwa jina la Nyumbani ambao Diamond na Alikiba walishiriki pia. Na kuna video ya Tunda Man 'Starehe Gharama' wawili hao wanaonekana pamoja, hivyo basi wawili hao wanaweza kufanya wimbo pamoja kwa sababu waliwahi kuwa na mahusiano mazuri hapo awali.
Bila shaka unakumbuka bifu la Prezzo na Jaguar kutokana Kenya lilivyoisha baada ya kusumbuana kwa kipindi kirefu, hawa hawakuwahi kufanya wimbo wowote hapo awali au kuwa pamoja kwenye chochote kile ila waliamua kumaliza bifu lao na kutoa wimbo unaokwenda kwa jina la Timika
Maoni