Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Ammy Ninje.
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Jumamosi Oktoba 20, 2018 Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala ilipitia masuala mbalimbali ikiwemo kumthibitisha Ammy Ninje katika nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.
Nafasi hiyo ilikuwa inakaimiwa na Oscar Milambo ambaye ataendelea na jukumu lake la Ofisa Maendeleo wa Vijana. Pia Kamati hiyo ya Utendaji imepitisha tarehe ya Mkutano Mkuu wa TFF wa mwaka ambao utafanyika Jijini Arusha Disemba 29, 2018.
Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na umepata siku 60 za kutangazwa kabla ya kufanyika.
Aidha kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimepitisha mabadiliko madogo kwenye kamati ndogo ndogo za TFF. Mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya Wajumbe kujiuzulu na wengine kukabiliwa na majukumu mengi.
KAMATI YA NIDHAMU
1. Kiomoni Kibamba - Mwenyekiti
2. Peter Hella - M/Mkiti
3. Kassim Dau - Mjumbe
4. Handley Matwenga - Mjumbe
5. Twaha Mtengera - Mjumbe
KAMATI YA RUFAA MAADILI
1. Richard Mbaruku - Mwenyekiti
2. Thadeus Karua - M/Kiti
3. Mh. Mussa Zungu - Mjumbe
4. Asp Benedict Nyagabona - Mjumbe
5. Lugano Hosea - Mjumbe
KAMATI YA UCHAGUZI
1. Malangwe Ally - Mwenyekiti
2. Mh. Mohamed Mchengela - M/Kiti
3. Benjamini Karume - Mjumbe
4. Mohamed Gombati - Mjumbe
5. Hamisi Zayumba - Mjumbe
Maoni