Mohammed Dewji ambaye ni mmiliki wa asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba.
Mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba Swed Mkwabi, ameweka wazi mipango yake na kuomba wanachama wa klabu hiyo wamchague.
Kampeni za uchaguzi huo wa Simba utakaofanyika November 4, 2018, zimefunguliwa rasmi jana, na leo Mkwabi ameweka wazi mipango yake kwa kusema atahakikisha pesa ya uwekezaji bilioni 20 itakayotolewa na Mohammed Dewji inaongezeka maradufu.
''Bilioni 20 ni pesa nyingi lakini inahitaji weledi mkubwa wa kuifanya endelevu, inaweza ikachotwa ndani ya miaka mitatu ikaisha tukashindwa kuzalisha tena tukarudi tulikotoka kwa hiyo kama nitapata fursa kwa kushirikiana na wenzangu tutatengeneza misingi ya kibiashara kuitoa katika bilioni 20 kuifanya iwe zaidi'', ameeleza.
Aidha Mkwabi amesema kuwa ameshagundua wanachama wa Simba wanataka wajumbe wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa ajili ya Simba na anaamini wanajua kuchuja mjumbe gani anafaa na yupi hafai hivyo hata akiwa mwenyekiti anajua atapata wajumbe bora.
Swedy Mkwabi mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa Simba
Mkwabi ambaye taaluma yake ni masomo ya biashara na masoko ameongeza kuwa anaamini ni wakati mwafaka wa yeye kutumia taaluma yake na uzoefu kuisaidia Simba.
Mkwabi amebaki peke yake kwenye nafasi hiyo baada ya hivi karibuni aliyekuwa mpinzani wake, Mtemi Ramadhani kujiondoa kwenye uchaguzi
Maoni