Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tambua njia za kufuata kuleta suluhu za mifarakano katika mahusiano




Migongano na tofauti kati ya watu wawili katika mahusiano ni kitu kisichoepukika iwe ni mahusiano ya mapenzi ,mahusiano ya mzazi na mtoto na hata mahala pa kazi. Sababu za mifarakano katika mahusiano ziko wazi;kwamba watu hawa wametoka na kukulia katikla mazingira tofauti na hivyo tabia na hulka zao ni lazima zitatofautiana. 

Katika hali kama hii migongano na kutoelewana wakati mwingine ni vitu ambavyo vinatokea na kunahitajika busara na mbinu mahususi za kukabiliana na tatizo hili 

Njia 7 Muhimu za Kutatua Mifarakano Katika Mahusiano 
1. Kuwa wa Kwanza Kuchukua Hatua 
Kunapotokea kufarakana kati ya watu wawili kwa kawaida mawasiliano huvunjika au kuwa magumu na mabaya. Kila mmoja anaweza akwa na kinyongo na mwingine. Kwa wapenzi hali hii inaweza ikawa ya kuumiza zaidi kwani inahusisha hisia kwa kiasi kikubwa;ni jukumu lako wewe kufunja ukimya na kuwa wakwanza kuleta suluhu. 

Tafuta nafasi na omba kujadili na kuongea kuhusu tofauti zenu. 

2. Anza Kwa Kuangalia Kosa Lako Kwanza 
Ni kawaida katika ugomvi na mifarakano kwa mmoja kumuona mwenzake kuwa ndiye mkosaji,na kusahau kuwa huenda kosa likawa upande wake pia. Kama suala hilo limemuudhi mwingine pia huenda kuna tatizo toka kwako pia,au labda yeye anaona kuna tatizo upande wako. 

Kutambua hilo unahitaji kujihakiki mwenyewe kwanza na kumsikiliza mwenzio kama ana hisia gani. Kama utaona kuna shida upande wako pia basi ni wakati wa kuomba msamaha kwa nafasi yako kwanza. 

3. Sikiliza kwa Umakini Shida na Mtazamo Toka Upande wa Pili-Vaa Viatu Vyake 
Inasemwa kuwa sababu kubwa ya malumbano na ugomvi ni kuwa tunataka kusema zaidi kuliko kusikiliza upande wa pili,na kwa kufanya hivyo tunakuwa wabinafsi. 

Ukisikiliza vizuri toka upande wa mwingine na kujaribu kusikia hisia zake huenda ukaliangalia jambo husika katika namna nyingine ambayo itapelekea maelewano. Ni muhimu sana kuonesha kuwa unajali hisia zake. 

4. Kuwa Mkweli na Maanisha Unachokisema-Sema toka Moyoni 
Mdomo unaweza kutamka chochote bila kumaanisha,kweli hutoka moyoni. Unaposema kitu kwa hisia na kwa dhati unasikika zaidi. Ongea toka moyoni na maanisha unachosema na matokeo yake yatakuwa mazuri. 

5. Jizatiti Katika Kusuluhisha Tatizo na Sio Kulaumu 
Lawama hazisaidii kuleta suluhisho la tatizo mbele yenu,ukweli ni kuwa linasababisha upande wa pili kujihami,ni asili kwa mtu anayeshambuliwa kujihami hali kadharika katika mazungumzo. 

Badala ya kulaumu ni vyema kama mtaangalia tatizo lenyewe ni nini na mzizi wake. 

6. Kazania katika Kupata Maelewano na Sio Kumaliza Tofauti Zote 
Si kitu rahisi mkamaliza tofauti zenu kwa kuwa ni watu wawili mliotoka katika mazingira yasiyofanana,badala yake mukubaliane namna ambazo mtaishi kwa amani na kuheshimu hisia na nafasi ya mwingine. 

Kuwa tayari kukubaliana kutokubaliana katika baadhi ya mambo. Maelewano ndio jambo la msingi katika kuleta suluhu. 

7. Kazania katika Kuonesha Kipi ni Sahihi na Sio Nani yuko Sahihi 
Katika mifarakano si vyema kumtaja mwingine kuwa hayuko sahihi,kwasababu ya kwanza ni kuwa huenda wewe mwenyewe ukawa hauko sahihi lakini ya pili ni kuwa huko ni kurusha makombora ya lawama ambako kutamfanya mwingine kujihami na hivyo kutofikia maelewano. 

 Jambo la Mwisho la Kuzingatia 
Mnapotafuta suluhisho la ugomvi au mfarakano katika mahusiano ni muhimu kuzingatia vitu viwili vikubwa,kuondoa ubinafsi na kujishusha. Kwasababu ukosefu wa vitu hivi viwili ndio sababu kubwa katika mifarakano yote. 

Na msingi upo katika kusikiliza hisia za mwingine. Usikivu ni bora zaidi kuliko kusema,unaposikiliza unaonesha kujali zaidi na inakuwa rahisi kufikia maelewano na kumaliza ugomvi na mifarakano katika mahusiano yoyote

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...