Kampuni ya Mintz Group inadai kuwa wafanyakazi wake watano walikamatwa na shughuli zake zikakoma, na wameapa "kusuluhisha kutoelewana" na mamlaka.
Biashara hiyo yenye makao yake makuu mjini New York - ambayo kwa mujibu wa tovuti yake inajishughulisha na ukaguzi wa nyuma, kukusanya ukweli na uchunguzi wa ndani - inadai kuwa haikupewa taarifa ya kisheria ya uvamizi huo, na inasema wafungwa wanazuiliwa bila mawasiliano nje ya Beijing.
"Tahadhari nyekundu zinapaswa kutolewa katika vyumba vyote vya mikutano hivi sasa kuhusu hatari nchini Uchina," mfanyabiashara mmoja wa Marekani aliiambia Reuters.
Maoni