MTEULE THE BEST
Mwizi mmoja nchini Guinea ameipongeza polisi kwa kumpata kwa njia ya video ambayo imeenea sana kenye mitandao ya kijamii ya habari.
Boubacar Diallo, mwanafunzi katika Chuo cha ufundi cha Mamou, na mwizi mwenzake wamekiri wenyewe kwamba waliiba kiasi cha franga milioni 50 pesa za Guinea sawa na dola 5,600; kutoka kwenye duka la simu eneo la kaskazini magharibi mwa mji huo.
Katika picha ya video alipokuwa amekamatwa na polsi zilizosambazwa , Diallo alitoa wito polisi wapewe raslimali zaidi za kazi yao.
"Mkuu wa polisi nchini humo anapaswa kupongezwa. Pia ninataka kusema kwamba polisi wanahitaji vifaa kwasababu polisi yetu ina maafisa wenye mafunzo mazuri, si mchezo ," alisema Diallo ambaye sasa yuko mikononi mwa polisi.
Ameongeza kuwa hakuwahi hata siku moja kufikiria kwamba anaweza kukamatwa haraka na akasema anajuta kwa uhalifu wake na akaapa kutoiba tena
Maoni