MTEULE THE BEST
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atakabiliana na makocha wengine kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale iwapo Real Madrid wanataka kumuuza.
Bale mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na mabingwa hao wa Uhispania kwa fedha za uhamisho zilizovunja rekodi ya £85m kutoka Tottenham.
Mabingwa wa ligi ya Yuropa Man United wanakutana na Real Madrid ambao walishinda kombe la vilabu bingwa Ulaya katika kombe la Supercup Jumanne.
''Iwapo atashiriki ni ishara tosha kwamba atasalia Madrid'', alisema meneja wa Real Madrid
Mourinho alisema kuwa iwapo Bale atashiriki katika mechi hiyo basi atakuwa katika mpango wa kocha wake na klabu na ni haki na mpango wake kusalia.Basi sitafikiria kumpigania.
''Iwapo hayupo katika mpango wa klabu na ni kweli mchezaji kama Bale anataka kuondoka nitajaribu kuwa hapo nikimsubiri upande mwengine''.
Bale aliimarisha kandarasi yake katika klabu hiyo mwaka uliopita akisema anafurahi kusalia na mabingwa hao mara 12 wa kombe la vilabu bingwa.
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 08.08.2017Paris Saint-Germain wapo tayari kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, na wanajiandaa kutoa pauni milioni 161 kumtaka mchezaji huyo anayesakwa pia na Real Madrid na Manchester City. PSG watamuuza Angel Di Maria ili kupata fedha zaidi za kukamilisha usajili huo. (Le Parisien)
Liverpool watapanda dau la pauni milioni 60 kumtaka Virgil van Dijk kufuatia hatua ya mchezaji huyo kuwasilisha rasmi maombi ya kutaka kuondoka Southampton. Chelsea pia wanamtaka beki huyo, ingawa Antonio Conte anataka zaidi kusajili mabeki wa pembeni huku Serge Aurier wa PSG akiwa miongoni mwao. (Express)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameghadhibishwa na matatizo ya beki wa PSG Serge Aurier ya kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza, na hivyo kuamua kuelekeza nguvu zake kumtaka Fabinho wa Monaco na anadhani dau la pauni milioni 45 litatosha kumshawishi. (Don Balon)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp atakataa mkataba wowote kuhusu Philippe Coutinho kuondoka Anfield kwenda Barcelona. (Daily Mirror)
Liverpool hawataweza kumzuia Philippe Coutinho, 25, kuondoka msimu huu amesema mkongwe wa klabu hiyo Greame Souness. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England Ian Wright amesema Philippe Coutinho “hana budi kwenda” Barcelona. (BBC Radio 5 Live)
Barcelona bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20. (Sport)
Manchester United watapanda dau kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 28, ikiwa mchezaji huyo ataachwa na Zinedine Zidane katika kikosi kitakachocheza fainali ya Uefa Super Cup. (Times)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane ametupilia mbali taarifa za Gareth Bale kurejea England. (Mirror)
Chelsea na Manchester United zote zitapanda dau kumtaka beki wa PSG Serge Aurier, 24. (Daily Mail)
Kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater anajiandaa kuiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka na kujiunga na Chelsea. (Mirror)
Eden Hazard yuko tayari kuondoka Chelsea na kujiunga na Real Madrid. (Don Balon)
Chelsea wana matumaini makubwa ya kumpata beki wa Southampton Virgil van Dijk kwa sababu ya uhusiano tete kati ya Liverpool na Southampton. (Telegraph)
Southampton wanapanga kumsajili beki wa kati wa Middlesbrough Ben Gibson, 24, kuziba nafasi ya Virgil van Dijk. (Sun)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amesema Arsenal walitakiwa kumsajili Nemanja Matic kutoka Chelsea kwa sababu timu hiyo inakosa kiongozi uwanjani. (BBC Radio 5 Live)
Manchester United na Inter Milan zimerejea tena kumtaka beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, 27. (Daily Mirror)
Manchester City wamemuulizia kiungo wa Barcelona Sergio Busquets. (Onda Cero)
Valencia wanajiandaa kupanda dau la kumshawishi beki wa Arsenal Gabriel, 26, kuhamia Uhispania. (Evening Standard)
Trabzonspor ya Uturuki inataka kumsajili kiungo wa Tottenham Moussa Sissoko, 27, kwa mkopo.
Maoni