Sehemu ya mabaki ya ndege
Kombora lililodungua ndege ya shirika la ndege la Malaysia mashariki mwa Ukrain mwaka 2014 lilikuwa na Urusi, wachunguzi wa kimataiafa wamesema.
Kwa mara ya kwanza timu ya wachunguzi ikiongozwa na Uholanzi imesema kombora hilo lilitoka kwa kikosi cha Urusi kilicho mji wa Kursk.
Watu wote 298 waliokuwa ndani ya ndege ya Boeng 777 waliuawa wakati ilivunjika vipande ikiwa safarini kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur.
Ilipigwa na kombora aina ya BUK lililofyatuliwa kutoka eneo lililodhitiwa na waasi nchini Ukrain. Urusi inasema hakuna silaha zake zilizotumika.
Sehemu ya mabaki ya ndege
Lakini leo Alhamisi Wilbert Paulissen, afisa wa Uholanzi kutoka kundi la wachunguzi la pamoja JIT, aliwaambia waandishi wa habari kuwa magari kwenye msafara uliobeba kombora hilo ulikuwa sehemu ya jeshi la Urusi.
Alisema wachunguzi walikuwa wamefuatilia msafara huo na kugundua kuwa ulikuwa wa kikosi wa 53 cha jeshi la Urusi
Kisa hicho kilitokea wakati wa mzozo kati ya serikali na waasia wanaoungwa mkono na Urusi.
Mwezi Oktoba mwaka 2015 kamati ya Uholanzi ilisema kuwa ndege hiyo iligongwa na kombora lililotengenezwa nchini Urusi la BUK.
Njia ambayo kombora hilo lilipitia
Maoni