Rais Donald Trump
Rais Donald Trump amesema Ijumaa asubuhi kuwa Korea Kaskazini imetoa mrejesho wa āukarimuā na āufanisi" baada ya kusitisha mkutano wake na Kim Jong Un.
āNi habari nzuri sana kupokea kauli ya mrejesho ya upole na ufanisi kutoka Korea Kaskazini,ā Trump amesema katika ujumbe wa Twitter Ijumaa asubuhi.
āHivi karibuni tutafahamu kile kitakachoendelea, ni matumaini yangu itakuwa ni utajiri na amani ya kudumu na ya muda mrefu. Ni wakati peke yake (na kipaji) utatuthibitishia hili.
Korea Kaskazini imesema Ijumaa bado iko tayari kufanya mazungumzo na Marekaniā wakati wowote, [katika] mpangilio wowote.ā
Makamu Waziri wa Mambo ya Nje Kim Kye Gwan, mwakilishi katika mazungumzo ya nyuklia wa muda mrefu na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu, amesema katika tamko lililotangazwa na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini iko ātayari kuipa Marekani muda na fursaā kufikiria suala la mazungumzo.
Trump alijitoa kufanya mkutano na Kim kama ilivyokuwa imepangwa Alhamisi asubuhi, akilaumu matamko yaliyotolewa na Pyongyang hivi karibuni yakitishia kutoshiriki katika mkutano huo kwa kile waliocho kiona ni kauli za mashambulizi ziliotolewa na maafisa wa Marekani
Mwanadiplomasia wa Korea Kaskazini amesema kauli kali za Pyongyang zilisababishwa na kujigamba kwa Marekani kulikopita kiasi, na uhasama uliojitokeza hivi sasa unaonyesha āumuhimu mkubwaā wa kuwepo mazungumzo hayo.
āJapokuwa tuko kimya tunaridhishwa na uamuzi wa kishujaa wa Rais Trump ambao hakuna rais yoyote wa Marekani aliwahi kujaribu kuchukua, na kufanya juhudi kuandaa tukio hilo muhimu la mkutano huo,ā tamko la Kim Kye Gwan limesema
Maoni