Ruka hadi kwenye maudhui makuu

RAIS WA MAREKANI AFICHUA SIRI KUU ZA IS KWA URUSI

MTEULE THE BEST



Mr Trump (kati) akifurahia jambo na Lavrov (kushoto) na Sergei KislyakHaki miliki RAIS wa Marekani Donald Trump alifichua taarifa zinazofaa kuwa siri kuu kuhusu kundi linalojiita Islamic State (IS) kwa waziri wa mambo ya nje wa urusi, vyombo vya habari nchini Marekani vinasema.
Taarifa hizo, zilihusu kutumiwa kwa laptopu kwenye ndege, na zilitoka kwa mshirika wa Marekani ambaye hakuwa ametoa idhini kwa habari hizo kukabidhiwa Urusi, gazeti la Washington Post linasema.
Bw Trump alikutana na Sergei Lavrov katika afisi yake wiki iliyopita.
Mshauri mkuu wa usalama wa taifa wa Marekani HR McMaster amepuuzilia mbali madai hayo kwenye vyombo vya habari na kusema ni ya "uongo".
Tuhuma kwamba huenda maafisa wa kampeni wa Bw Trump waliwasiliana na maafisa wa Urusi zimegubika utawala wa rais huyo, na kufikia sasa uchunguzi unaendelea
Lakini rais amepuuzilia mbali tuhuma hizo na kusema ni "habari za uongo".
Wakati wa kampeni, Bw Trump alimkosoa sana mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton, kwa jinsi alivyoshughulikia taarifa ambazo zinafaa kuwa siri kuu.

Nini hasa kilitokea?

Katika mazungumzo yake na Bw Lavrov pamoja na balozi wa Urusi nchini Marekani katika afisi yake White House, trump alifichua maelezo ambayo huenda yakapelekea kutambuliwa kwa mdokezi aliyetoa habari hizo, maafisa waliambia Washington Post na New York Times.
Walizungumzia njama ya IS. Rais huyo inadaiwa alianza kuzungumzia mambo ambayo alikuwa hajapangiwa kuyazungumza, na kufichua maelezo zaidi kuhusu njama hiyo.
Njama hiyo inadaiwa kujumuisha kutumiwa kwa laptop kwenye ndege. Mazungumzo ya trump yaligusia ni jiji gani kulikuwa kumegunduliwa tishio.
Habari hizo za kijasusi zilitoka kwa mshirika wa Marekani na zilichukuliwa kuwa za usiri mkubwa kiasi kwamba hazikufaa kufahamishwa washirika wengine wa Marekani, magazeti hayo yameripoti.
Wengine waliokuwepo katika mkutano huo waligundua kosa hilo la Bw Trump na wakachukua hatua kujaribu kuzima moto huo kwa kuwafahamisha maafisa wa CIA na maafisa wa Shirika la Usalama wa taifa (NSA), gazeti la Washington Post linasema.
Hatua ya Bw Trump si kwamba ni kinyume cha sheria, kwani Rais wa Marekani ana uhuru wa kuamua ni habari gani zitaorodheshwa kama siri kuu na gani hazitaorodheshwa kama siri kuu.
Mkutano huo ulitokea siku moja baada ya Bw trump kumfuta kazi mkuu wa FBI James Comey, hatua iliyoshutumiwa vikali kwamba FBI walikuwa tayari wanachunguza uhusiano wa maafisa wa kampeni wa Bw Trump na maafisa wa Urusi.

White House wamesema nini?

Mshauri mkuu wa usalama wa taifa HR McMaster ameambia wanahabari kwamba taarifa hizo, kama zilivyoripotiwa na magazeti hayo mawili, ni za uongo.
"Rais na waziri huyo wa mambo ya nje walizungumza kuhusu hatari mbalimbali zinazokabili nchi hizi mbili, zikiwemo hatari katika sekta ya uchukuzi wa kutumia ndege,2 alisema.
"Haikutokea - hata wakati mmoja - ambapo duru za kijasusi au njia za kupokea habari zilizungumziwa. Na rais hakufichua shughuli zozote za kijeshi ambazo kufikia sasa hazifahamiki na umma 
Kupitia taarifa, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alikariri hilo na kusema maelezo ya ndani kuhusu "hatari mbalimbali" hayakuzungumziwa na kwamba wadokezi, njia au operesheni za kijeshi havikujadiliwa.
Gazeti la Washington Post, ambalo lilichapisha habari hizo kwanza, lilisema hilo si kukanusha taarifa hizo.
Mwanahabari Greg Jaffe aliambia BBC kwamba gazeti la Post liliweka wazi kwamba rais hakuzungumzia wadokezi wala njia za kupata habari hizo za kijasusi

Lakini akaongeza: "Taarifa yetu ilizungumzia habari zenyewe ambazo zingewezesha Warusi kurudi nyuma na kufuatilia na kuweza kujua wadokezi na njia zenyewe. Alisema mengi sana kiasi kwamba wanaweza kujua hayo (mdokezi na njia hizo)." 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...