Haak Hayik mchezaji soka mkongwe duniani
Mchezaji wa soka wa Israel, Isaak Hayik aliye na miaka 73 amevunja rekodi ya kuwa mwanasoka mkongwe zaidi duniani.
Isaak aliandikisha historia hiyo baada ya kucheza kama mlinda lango wa timu ya Israeli ya Ironi ama Yehuda siku ya Ijumaa.
Licha ya umri wake mkubwa, Hayik alisema "yuko tayari kwa mchezo mwingine" baada ya kucheza kwa dakika 90.
Amepokea tuzo ya Guinness World Records katika hafla iliyoandaliwa baada ya mechi hiyo, siku kadhaa kabla ya sherehe 74 ya kuzaliwa kwake.
Japo timu yake ilifungwa mabao 5-1 na timu ya Maccabi Ramat Gan, mzaliwa hiyo wa Iraq anasemakana kuwa alionesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo.
"Hii sio fahari yangu pekee bali ni fahari ya Israel michezoni kwa ujumla," Hayik aliliambia shirika la habari la Reuters.
Mmoja wa watoto wake wa kiume Moshe Hayi, aliye na umri wa miaka 36, alisifia ufanisi wa baba yake kwa furaha na bashasha"siamini kwa kweli", alisema.
Haki miliki ya pichaREUTERS
Alitania jinsi baba yake alivyokuwa akimshinda maarifa "nilikuwa nikichoka mbele yake" tukicheza pamoja.
Raia wa Uruguay Robert Carmona, aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo alikua na miaka 53, na alikua akicheza katika kikosi cha kwanza cha timu ya Pan de Azucar mwaka 2015.
Raia wa Japan, Kazuyoshi Miura, ndiye alikuwa mshambuliaji mkongwe zaidi kuwahi kufunga bao katika mashindano ya kandanda.
Alivunja rekodi ya Sir Stanley Matthews, 52, mwaka 2017 baada ya kuifungaa Yokohama FC bao 1-0 katika mechi yake dhidi ya Thespa Kusatsu iliyokuwa ikishiriki Ligi ya daraja la pili
Maoni