Beki wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Baroka FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini, Abdi Banda amesema mwaka huu ana mpango wa kufungua kituo cha kukuza vipaji vya soka mkoani Tanga.

"Malengo yangu ni kuwasaidia vijana wenzangu wa Kitanzania na mwaka huu natarajia kufungua kituo cha kukuza vipaji jijini Tanga," amesema Banda.
Banda amesema atafanya hivyo kwasababu anatambua kuwa wapo vijana wengi ambao wana ndoto za kufika mbali zaidi kisoka, hivyo wanahitaji msaada kutoka kwa watu ambao wapo mbele katika soka.
''Unapocheza nje ya Tanzania ni vizuri kuonyesha mchango wako kwa vijana walio chini yako, kwahiyo hilo ndio lengo langu na sitaishia tu kujenga kituo nitaendelea kutoa vifaa vya michezo kwaajili ya vijana wenye ndoto za kuwa wachezaji wakubwa'', ameongeza.

Maoni