MTEULE THE BEST
George Weah alikuwa mchezaji Monaco Wenger alipokuwa meneja
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameambia BBC kwamba amepokea mwaliko kutoka kwa rais mteule wa Liberia George Weah kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwake baadaye mwezi huu.
Wenger amesema: "Nimealikwa na George kwa siku hiyo ambapo ataapishwa kuwa Rais."
Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais.
"Maisha ya jamaa huyu kwa kweli ni kama filamu. Ni ya kushangaza. Yanaweza kuunda filamu nzuri sana," amesema Wenger.
"Nakumbuka nilipomuona mara ya kwanza Monaco alipofika na alikuwa anaonekana kukanganyikiwa kidogo, hakuwa anamjua mtu yeyote, na hakuwa anatazamwa na wengi kama mchezaji stadi na baadaye akaibuka na kuwa mchezaji bora duniani 1995 na leo hii sasa amekuwa rais wan chi. Ni kisa cha kushangaza," Wenger ameongeza.
Wenger amesema Weah kwa muda mrefu amekuwa anaipenda sana nchi yake na ana ukakamavu ambao umemfanya kuamini kwamba alikuwa na ndoto fulani maishani.
"Nilisafiri na George wakati huo kulipokuwa na vita nchini Liberia na nimeona jinsi alivyotatizika kutokana na taifa lake na hilo lilikuwa jambo moja ambalo lilikuwa linaendelea kwa muda taifa lake, upendo wake kwa taifa hilo na watu wake," amesema Wenger.
"Leo hii nikitazama nyuma na kumuona akitokwa na machozi vita vilipokuwa vimechacha Liberia ni jambo la kufurahisha sana na natumai atakuwa rais wa furaha na ningependa kuona bwana huyu akiwa mfano mzuri kwa wachezaji wote wa soka wa sasa."
Wenger amesema kwamba hataweza kusafiri Liberia kuhudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Weah kutokana na shughuli nyingi Ligi ya Premia.
Wenger alikuwa mkufunzi wa George Weah miaka ya 1990 Monaco
"Ninaamini nitakuwa na shughuli nyingi lakini iwapo nitapigwa marufuku basi nitapata muda wa kwenda," Wenger, ambaye amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu na Chama cha Soka England amesema.
Weah alishinda duru ya pili ya uchaguzi mwezi jana dhidi ya aliyekuwa makamu wa rais Joseph Boakai kwa kupata zaidi ya 60% ya kura.
Atachukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika
Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi. Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria. Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao. Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...
Maoni