Mshukiwa aliyeabiri ndege kisiri inaaminika ameanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, na kuanguka katika bustani moja huko kusini mwa London
Lakini ni mara ngapi visa kama hivyo huhuhudiwa na hali huwa vipi wakati wa safari za aina hiyo?
Ni mara ngapi visa hivi hutokea?
Licha ya kwamba sio jambo la kawaida, hii sio mara ya kwanza kwa mtu kuingia katika sehemu za ndege wakati ndege hiyo ikisafiri na kujificha wakati wa safari ya kuelekea Uingereza.
mwili ulipatikana katika bustani ilioko Offerton Road huko Clapham
Kati ya Januari 2004 na Machi 2015, watu sita walioingia kwa siri katika ndegekatika uwanja wa ndege Uingereza walipatikana kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za shirika la viwanja vya ndege (CAA). Mwingine mmoja alipatikana katika ndnai ya ndege ya Uingereza katika uwanja wa ndege ng'ambo.
Takwimu kutoka shirika la viwanja vya ndege Marekani zimeashiria kuwa watu 96 wamewahi kujificha katika sehemu za ndege wakati ndege zikiwa safarini kote duniani kati ya mwaka 1947 na 2012, huku kukiwa na visa katika ndege 85.
Ni wangapi waliofariki?
Kumeshuhudiwa visa kadhaa vya watu kujificha na kutoroka katika ndege waliopatikana wamefariki Uingereza.
Mnamo 2001, mwili wa Mohammed Ayaz, mwenye umri wa miaka21, kutoka Pakistan, ulipatiakana katika enoe la kuegesha magari huko Richmond, karibu na uwanja wa ndege wa Heathrow.
Miaka minne awali mtu mwingine aliyejificha kwenye ndege alianguka kutoka juu hadi katika eneo la kuuza gesi.
Mnamo 2007 mwili wa kijana mmoja ulipatikana katika gia ya ndege ya British Airways huko Los Angeles.
Mnamo Agosti 2012, mwili wa mwanamume ulipatikana katika eneo la kuweka mizigo la ndege katika uwanaj wa Heathrow baada ya kuwasili kwa ndege kutoka Cape Town. Mwezi uliofuata, Jose Matada, mwenye umri wa miaka 26,kutoka Msumbiji, alipatikana katika mtaa mmoja huko Mortlake, London magharibi. Alifariki kutokana na majeraha mengi baada ya kuanguka kutoka kwenye ndege kutoka Angola.
Mnamo Juni 2015, mwanamume mmoja alipatikana amefariki juu ya paa la ofisi moja huko Richmond. Mwingine alipatakana katika hali mahututi Heathrow. Inadhaniwa walining'inia kutoka kwenye ndege ya British Airways iliotoka Johannesburg.
Wanaoponea mara nyingi huwa wamesafiri safari fupi na wengi wao huwa ni vijana.
Ndege yaanguka katika paa la nyumba Marekani
Kati ya visa vilivyobainika Marekani, watu 23 - mmoja kati ya wanne walinusurika katika safari hizo.
Miongoni mwa walioponea
1969 - Armando Socarras Ramirez, 22, alinusurika katika safari kutoka Havana, Cuba, kwenda Madrid, alipigwa na baridi kali lakini hakuathirika pakubwa.
1996 - Pardeep Saini, 23, alinusurika katika safari ya saa 10-kutoka Delhi kwenda London, lakini kakake Vijay alifariki baada ya kuanguka kutoka kwenye ndege ilipokaribia Heathrow
2000 - Fidel Maruhi alinusurika safari ya maili 4,000katika ndege ya Boeing 747 kutoka Tahiti hadi Los Angeles
2002 - Victor Alvarez Molina, 22, alinusurika katika safari ya saa nne katika ndege ya DC-10 kutoka Cuba kwenda Montreal, Canada
2014 - Yahya Abdi, 15, alitoroka kwenye ndege ya Boeing 767 kutoka San Jose, California, hadi Maui, Hawaii
Nini kinachotokea wakati wa safari ya ndege?
Kuna hatari kubwa inayowakabili watu wanaosafiri katika sehemu ya chini ya ndege.
hii ikiwa ni pamoja na kukanyagwa wakati gia za kutuwa ndege zinapofunguka, baridi kali, kupoteza uwezo wa kusikia na kuwepo tindi kali mwilini inayoweza kusababisha mtu kupooza au hata kufariki.
Wakati wa safari, hali ya ujoto inaweza kushuka hadi kupungua -63C.
Kwa urefu wa futi 18,000 mwili unakosa hewa ya kutosha na kusababisha hali ijulikanayo kama hypoxia. Husababisha mwili kulemaa, kutetemeka, mtu kusikia kisunzi na hata mara nyingine kupata matatizo ya kuona.
Wakati ndege inapofika futi 22,000 angani mtu aliyejificha katika sehemu za ndege atakuwa anajitahidi asipotewe na fahamu kutokana na kwamba viwango vya oxygen ndani ya damu hushuka.
Kuna hatari kubwa inayowakabili watu wanaosafiri katika sehemu ya chini ya ndege
Alafu milango ya sehemu za ndege hufunguka futi elfu kadhaa angani kabla ya ndege kutuwa., jambo linaloweza kuwasababisha watu kuanguka na kufariki.
Wanaingia vipi kwenye ndege hizo?
Mara nyingi tatizo huwa ni usalama katika uwanja wa ndege.
Watu hufanikiwa kuingia katika ndege hizo iwapo usalama haujaimrishwa vilivyo.
katika kisa cha jamaa aliyefariki mnamo Agosti 2012 baada ya kuingia kwenye ndege kwa siri kutoka Cape Town kwenda London, tahadhari ilitolewa kuchelewa.
Maafisa wa ndani ya ndege waliarifiwa wakati wa safari hiyo kuwa kuna mtu aliyeonekana akiingia katika sehemu ya chini ya ndeg
Maoni