
Gareth Bale
Manchester United wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale,30, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Sun on Sunday)
Paris St-Germain wanawezekana kuwa kikwazo kikubwa kwa mpango wa Manchester United wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19 mwenye thamani ya pauni milioni 120. (Sunday Express)
PSG pia wanamtaka kiungo wa Liverpool Adam Lallana,31.(Sunday Mirror)
Manchester United wanamtazama kwa karibu winga wa West Bromwich Albion Matheus Preira, anayecheza kwa mkopo akitokea Sporting Lisbon. (Mirror)

Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho
Arsenal wanajiandaa kumuwania mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uturuki, ambaye anaweza kuuzwa na Juventus kama ofa ya kuridhisha itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.(Tuttosport - in Italian)
Barcelona wanajadili mkataba mpya na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa zamani wa LA Galaxy na Manchester United Zlatan Ibrahimovic,38, anataka karibu pauni 900,000 kwa mwezi kurejea Serie A, ambako ameichezea Juventus, Inter Milan na AC Mian. Milan, Bologna na Napoli ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili mchezaji huyo.(Mail on Sunday)
Everton inamuwinda mshambuliani wa Eintracht Frankfurt Goncalo Paciencia, 25, mwezi Januari baada ya kocha Marco Silva kuitaka klabu kumsajili mshambuliaji.(Goal)

Lionel Messi
Roma inapaswa kuilipa Manchaster United pauni milioni 18 kama wataamua kubaki moja kwa moja na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling,29. (Tuttosport, via Metro)
Tottenham Hotspur itatoa ofa ya ongezeko la mshahara kwa mkataba wa miaka mitatu kwa mshambuliaji Troy Parrott. (Football Insider)
Bruno Fernandes,25, ambaye amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United na Real Madrid, amesema anafurahia kuwa Sporting Lisbon. (Goal)
Mshambuliaji wa Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku,26, amedai kuwa kocha wa Manchester United anamtaka kubaki Old Trafford.(Mail on Sunday)
Maoni