Ruka hadi kwenye maudhui makuu

CORONA| EPL, LIGUE 1, BUNDESLIGA, LALIGA, UEFA, UUROPA , ITALY, N.K ZASIMAMISHWA


Coronavirus: Mechi za Ligi ya soka ya England kuahirishwa hadi tarehe 3 Aprili








Mechi za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi tarehe 3 Aprili kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona.



Mashindano yote Ligi ya soka ya Ulaya, mkiwemo Championi Ligi na Ligi ya Ulaya, mechi ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus.

Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa.

Katika Championi Ligi, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa.

Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa.

Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa.

Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae".


Klabu ya Juventus imetangaza kwamba beki wa kati wa Italia Daniele Rugani amekutwa na virusi vya corona, na sasa amejiweka katika karantini

Bodi ya Soka ya Ulaya imewaalika wawakili wa wajumbe wa mashirikisho yote 55 kwa mkutano siku ya JUmanne ili kujadili mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa coronavirus.

Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa.

Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na18 Machi pia zimesitishwa.

Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae".

Bodi ya Soka ya Ulaya imewaalika mawakili wa wajumbe wa mashirikisho yote 55 kwa mkutano siku ya JUmanne ili kujadili mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa coronavirus.

Uefa imesema kuwa maamuzi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae".


Mpangilio wa Euro 2020 utajadiliwa katika mkutano huo.

Zaidi ya watu 125,000 wamepatikana na virusi vya corona katika nchi 118 kote duniani, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO. Idadi kamili ya vifoo vya watu ni zaidi ya 4,600.

Mechi zilizoahirishwa (zilizotarajiwe kuchezwa kati ya 17-19 Machi)

Champions League:

Bayern Munich dhidi ya Chelsea

Barcelona dhidi ya Napoli

Man City dhidi ya Real Madrid

Juventus dhidi ya Lyon


Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta na mchezaji wa Chelsea Callum Hudson Odoi wana virusi vya corona


Winga wa Chelsea Callum Hudson Odoi pia amepatikana na virusi vya corona

Europa Ligi:

Bayer Leverkusen dhidi ya Rangers

Getafe dhidi ya Inter Milan

Shakhtar Donetsk dhidi ya Wolfsburg

Wolves dhidi ya Olympiakos

FC Basel dhidi ya Eintracht Frankfurt

FC Copenhagen dhidi ya Istanbul Basaksehir

Manchester United dhidi ya LASK

Roma dhidi ya Sevilla


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...