LIVERPOOL KUWEKA KAMBI UJERUMANI SIKU 8

MTEULE THE BEST

Kikosi cha Liverpool tayari kimewasili mjini Munich Ujerumani ambako kitakaa kwa siku nane  nchini humo kikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka ya England.
Wakiwa huko, majogoo hao wa jiji chini ya kocha mkuu,  Mjerumani Jurgen Klopp watashiriki kombe dogo la AUDI CUP ambalo litajumuisha wenyeji wao mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich, miamba ya Hispania, Atletico Madrid na Napoli ya Italia.
Liverpool itasafiri kwenda Berlin kucheza mechi ya kirafiki Julai 29 mwaka huu dhidi ya Hertha Berlin, kabla ya kurejea Munich kutupa karata ya kwanza katika mashindano ya AUDI CUP ambapo itaanza kibarua kwa kuwavaa Bayern Munich Agosti mosi mwaka huu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU