Marekani kuziwekea wikwazo Urusi, Iran na Korea Kaskazini

MTEULE THE BEST
Baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.
Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiadhibiwa kufuatia majaribio ya makombora.
    Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili audhinishe na kuwa sheria kamili.
    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anashutumiwa kwa kuibua silaha hatarishi za nyuklia kila kukicha
    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anashutumiwa kwa kuibua silaha hatarishi za nyuklia kila kukicha
    Akizungumza katika baraza hilo wawakilishi David Ciciline kutoka chama Democratic amesema hatua kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi.
    Amesema hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita.
        Naye Ted Poe kutoka chama cha Republican amesisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea kaskazini pia.
        Rais wa Iran Hassan Rouhani ameahidi kuondoa migogoro ya kimataifa inayoikabili nchi hiyo
        Rais wa Iran Hassan Rouhani ameahidi kuondoa migogoro ya kimataifa inayoikabili nchi hiyo
        Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya bunge la Urusi Duma , Leonid Slutsky amesema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya Urusi na Marekani.

        Maoni

        Machapisho maarufu kutoka blogu hii

        ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

        MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

        KUMTUMAINIA MUNGU