BAKHRESA; apewa hekta elfu 10 na Rais MAGUFULI

MTEULE THE BEST

Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amempa hekta elfu 10 mwenyekiti wa makampuni ya chakula ya Bakhresa ,kulima miwa na kuazisha kiwanda cha sukari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa wakwanza (kulia), Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega wakivuta kamba kwa pamoja kuashiria ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusindika Matunda cha Bakhresa Mwandege mkoani Pwani
Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amempa hekta elfu 10 mwenyekiti wa makampuni ya chakula ya Bakhresa ,kulima miwa na kuazisha kiwanda cha sukari ili kukidhi soko la sukari ya nyumbani na viwandani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali serikali na menejimenti ya Bakhresa Group
Akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kampuni ya BAKHRESSA  FOOD PRODUCTS COMPANY baada ya kuzindua kiwanda cha kusindika matunda cha AZAM,RAIS MAGUFULI amesema suala la sukari ni jambo mtambuka na kuwa ni wakati sasa wawekezaji wazalendo wazalishe sukari ya viwandani hapa nchini ili kukuza pato la taifa na kuongeza ajira kwa vijana.
Awali akisoma risala ya kampuni kwa rais mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za BAKHRESA ABOUBAKARI BAKHRESA  amesema changamoto kubwa wanazokutana nazo katika kutimiza wajibu wao ni umeme,wingi wa taasisi za udhibiti wa ubora,na tozo nyingi.
Kiwanda cha kusindika matunda cha BAKHRESA kimegharimu dola za kimarekani milioni 100 na kinatoa ajira kwa watanzania takribani mia tisa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU