Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yuko nchini Saudi Arabia katika ziara isiyopanga, amesema atasisitizia umuhimu wa utulivu nchini Lebanon, katika mazungumzo yake na na viongozi wa nchi hiyo.
Ufaransa ina uhusiano wa karibu na Lebanon, na ziara hiyo ya Rais Macron imekuja siku moja baada Waziri mkuu Saad Hariri, kujiuzulu wakati alipokuwa Riyadh, hali inayochochea hisia kwamba alishinikizwa na Saud Arabia.
Awali akizungumza mjini Dubai, Rais Macron amesema anataka viongozi wa Lebanon kuishi huru ndani ya nchi yao.
Amesema pia atautaka uongozi wa Saud Arabia kusaidia kuzuia baa la njaa nchini Yemen, ambako muungano wa majeshi yanayoongozwa na nchi hiyo yamefunga bandari kuzia silaha kuingizwa nchini humo na kuwafikia wapiganaji wa Ki Houthi.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni