Wanasayansi nchini Uingereza wamegundua kwamba majeraha ya kukatwa na kuchomeka hupona haraka yanapopatikana mchana ikilinganishwa usiku.
Wanasema kwamba ni kutokana na mwili unavyohisi kulingana na muda.
Utafiti huo unasema kuwa seli za ngozi ya mwanadamu hubadilisha tabia yake kulingana na muda huku protini zinazohitajika kurekebisha majeraha hayo zikifanya kazi vizuri wakati wa mchana.
Jeraha la kuchomeka nyakati za usiku lilichukua siku 28 kupona ikilinganishwa na siku 17 za jereha la wakati wa mchana.
Watafiti walitaja tofauti hiyo kuwa kubwa huku wakiongezea kwamba wanaweza kuharakisha watu kupona kwa kutumia dawa za steroids ambazo hubadilisha muda wa mwili.Utafiti: Mbwa mwitu hufanya uamuzi kwa kupiga chafya
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Sayansi uliwahoji wagonjwa 118 katika kitengo cha wagonjwa waliochomeka nchini Uingereza.
Ulionyesha muda wa kupona wa 11 kati ya watu nyakati za mchgana na usiku.
Matokeo ya mahabara yalionyesha kuwa seli za ngozi kwa jina Fibroblast zilikuwa zikibadili uwezo wake katika kipindi cha saa 24.
Seli hizo ndizo za kwanza zinazokimbia katika jeraha hilo ili kufunga kidonda.
Nyakati za mchana huwa zinafanya kazi sana na hupoteza nguvu hiyo nyakati za usiku.
Daktari O'neil mmoja ya watafiti aliambia BBC ''ni kama kukimbia mita 100''. Mkimbiaji hujiandaa kutoka , kawaida atamshinda yule aliyesimama akijiandaa kukimbia''.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni