Papa Francis apiga marufuku uuzaji wa sigara Vatican






Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage caption
Licha ya sigara kuiletea mamilioni ya fedha Vatican ,papa Francis amesema kuwa hawezi kuruhusu binaadamu kuathiriwa kiafya

Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao.

Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.

Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei .


Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka.

Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.



Mtoto amvua kofia Papa Francis

Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.

''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.

''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.

Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa wakati alipokuwa kijana havuti sigara.

Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU