David Rudisha ni 'afande' Kenya
MTEULE THE BEST
Je wajua kuwa bingwa wa dunia wa
mbio za mita 800 za wanaume David rudisha ni afisa mkuu wa polisi nchini
Kenya? maelfu ya mashabiki wake walipigwa na butwaa alipochapisha picha
yake akiwa amevalia sare rasmi ya kikosi cha utumishi kwa wote katika
ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.
Bingwa huyo na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 800 kwa upande wa wanaume ni afisa mkuu wa polisi
Sio aghalabu kuwa bingwa huyo na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 800 kwa upande wa wanaume ni afisa polisi, asilimia kubwa ya wanariadha wakenya ni maafisa wa idara mbali mbali za vikosi vya ulinzi.
Wakenya wengi walisambaza picha hiyo katika mitandao ya kijamii.
Hata hivyo Rudisha alichapisha ujumbe huo akiwarai mashabiki wake kote duniani wajivunie kazi zao.
Rudisha akijumuika na mwanawe katika zoezi
Aidha ametumika katika matangazo mengi tu ya kibiashara.






Maoni