Ahukumiwa kwa kutembea kutoka Ufaransa hadi Uingereza

MTEULE THE BEST

 

Mwanamame mmoja raia wa Sudan amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na mahakama moja nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kutembea kwa miguuu kutoka nchini Ufaransa hadi Uingereza akipitia kwa reli
Abdul Rahman Haroun, ambaye alikiri mashtaka hayo alikuwa amepewa hifadhi nchini Uingereza mwaka uliopita.
Mwanamme huyo wa umri wa miaka 40 anaaminika kutembea umbali wa kilomita 50 kutoka Calaisin nchini Ufaransa, hadi Folkestone nchini Uingereza kabla ya kupatikana tarehe 4 mwezi Agosti mwaka uliopita.
Hata hivyo hawezi kufungwa jela kutoka na kipindi ambacho tayari amekuwa kizuizini.

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU