Uhuru Kenyatta ameahidi kukabiliana na ufisadi wakati alipochaguliwa kwa mara ya kwanza 2013
Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya watalazimika kupimwa kwa kutumia kifaa cha kuwafichua watu waongo ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi , rais Uhuru Kenyatta amesema.
Bwana Kenyatta alisema kuwa kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyikazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo.
Alikuwa akizungumza baada ya kufichuliwa kwamba shilingi dola bilioni 8 za Kenya zilipotea katika kitengo kimoja cha serikali.
Takriban wafanyikazi 40 wa umma wanakabiliwa na mashtaka kufuatia kashfa hiyo.
Kashfa hiyo ya ufisadi , ambayo ilifichuliwa na wauzaji bidhaa ambao walikuwa hawajalipwa , ilipelekea kuibiwa kwa fedha hizo katika shirika la vijana wa huduma kwa jamii NYS kupitia vyeti bandia na malipo ya ziada.
Uchunguzi huo wa NYS -ukiwa mpango muhimu wa serikali ya rais Kenyatta kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umeonekana kama pigo kwa ahadi ya rais huyo kukabiliana na ufisadi aliotoa wakati alipochaguliwa kwa muhula wa kwanza 2013.
Hotuba ya rais Kenyatta ni jaribio la kukabiliana na tatizo hilo ambalo kwa sasa 'limemea pembe'.
Kashfa hiyo ya ufisadi ilifichuliwa na wauzaji bidhaa ambao walikuwa hawajalipwa
Akihutubia makundi ya raia waliokutana kusherehekea miaka 55 tangu Kenya ijipatie Uhuru , amesema kuwa Kenya italazimika kuangamiza ufisadi kabla ya jinamizi hilo kuangamiza ufanisi na siku za usoni za vizazi vijavyo.
''Wacha nitaje mpango mmoja ambao tunapanga kuidhinisha kukabiliana na ufisadi'', alisema.
''Kama hatua ya kwanza , wakuu wote wa idara za kutoa zabuni na zile za hesabu katika wizara za serikali watafanyiwa ukaguzi mpya ikiwemo kupimwa na kifaa cha kuwatambua watu waongo ili kujua maadili yao''.
''Wale watakaofeli watasimamishwa kazi''.
Maoni