Dereva wa timu ya Red Bull Daniel Ricciardo, ameibuka mshindi wa mbio za magari duniani 'Formula One' kwenye mji wa Monaco nchini Ufaransa akiwabwaga nguli Lewis Hamilton wa Mercedes na Sebastian Vettel wa Ferrari.
Mbio hizo ambazo zimemalizika jioni hii Daniel Ricciardo amefanikiwa kuongoza katika mbio zote kwa mara ya kwanza akianza na mbio za majaribio ambapo alifanya hivyo jana na leo kwenye mbio kuu ameibuka kinara.
Nafasi ya pili kwenye mbio za Monaco Grand Prix leo imeshikwa na Sebastian Vettel huku nafasi ya tatu ikishikwa na bingwa mtetezi Lewis Hamilton ambaye alishika namba moja kwenye mbioz za Barcelona GP mwezi uliopita.
Baada ya kuongoza leo, Ricciardo sasa amepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa madereva msimu huu, akifikisha alama 72 kwenye mbio 7 ambazo tayari zimeshafanyika.
Nafasi ya kwanza bado inashikiliwa na Lewis Hamilton akiwa na alama 110 huku nafasi ya pili akiendelea kuwepo Sebastian Vettel akiwa na alama 96. Mbio zinazofuata ni katika miji mbalimbali huko Canada (Canadian Grand Prix).
Maoni