Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 31.07.2017

MTEULE THE BEST

Jose Mourinho amesema Nemanja Matic, 28, ā€œanataka sanaā€ kuondoka Chelsea na kujiunga na Manchester United. Tayari United wamekubali kutoa pauni milioni 40 na wanatarajia kukamilisha usajili huo siku chache zijazo. (Sky)

Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier amekubali kujiunga na Manchester United, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ameruhusiwa kuondoka na meneja Unai Emery. (Sky Sports)

Alexis Sanchez anafikiria kuwasilisha ombi la kuondoka Emirates ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. Sanchez anataka sana kuondoka, na Pep Guardiola yuko tayari kufanikisha usajili wake. Sanchez anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, na Arsenal wako tayari kutoa 300,000. (Daily Mirror)

Southampton wana matumaini kuwa Virgil van Dijk atabadili mawazo na kurejea mazoezini na kikosi cha kwanza wiki hii. Southampton hawataki kumuuza beki huyo anayenyatiwa na Liverpool. (Daily Echo)

Barcelona huenda wakaamua kumgeukia Mesut Ozil, 28, iwapo watashindwa kumpata kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho. Huku hatma ya Neymar kwenda PSG ikiwa inazungumzwa, Barca wanatafuta mchezaji wa kuziba pengo lake. (Don Balon)

Cristiano Ronaldo hataki Real Madrid imnunue Kylian Mbappe kwa sababu huenda kinda huyo ā€˜akamfunikaā€™ na kuathiri nafasi ya kushinda Ballon dā€™Or. (Diario Gol)

Matumaini ya Liverpool kumsajili Naby Keita yanazidi kupata wakati mgumu baada ya Inter Milan nayo kuingia katika harakati za kumtaka kiungo huyo. (CalcioMercato)

Arsenal na Tottenham wamepeleka maskauti wao kumtazama mshambuliaji kinda wa Caen, Yann Karamoh, ambaye ametajwa kuwa kama ā€œKylian Mbappe mwingineā€. Chipukizi huyo anafuatiliwa pia na Forentina na AC Milan na Inter Milan. (Sunday Mirror)

Chelsea wanapanga kutaka kumchukua kinda wa Celtic, Karamoko Dembele, 14. (The Sun)

Kiungo wa Everton Ross Barkley atalazimika kupunguza mshahara anaotaka iwapo anataka kujiunga na Tottenham ambao wapo tayari kumlipa pauni 120,000 kwa wiki, sawa na ambazo amezikataa Everton. (Mirror)

Everton watashikilia bei ya pauni milioni 35 kumuuza Ross Barkley licha ya kuwa mkataba wake utamalizika baada ya mwaka mmoja. (Mail)

Barcelona watawashitaki PSG kwa UEFA kwa kukiuka kifungu cha fedha hata kama hawatolipa pauni milioni 197 za kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar. (El Larguero)

PSG wana uhakika wa kumsajili Neymar, na tayari wanapanga jinsi ya kumtambulisha mchezaji huyo kwa mashabiki. (ESPN)

West Brom wanamtaka beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen, 31, ambaye alihamia Barcelona miaka mitatu iliyopita. (Sky Sports)

Meneja wa Bacelona Ernesto Valverde anataka kumpa namba Thomas Vermaelen msimu huu baada ya kufurahishwa na kiwango alichoonesha kwenye mechi za kujipima nguvu. (AS)

Wachezaji wa Manchester City wanazungumzia waziwazi kuwasili kwa Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa mkataba wa pauni milioni 50. (Manchester Evening News)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema wachezaji kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambao wanaingia katika mwaka wa mwisho wa mikataba yao ndio ā€œwazuri zaidiā€ kwa sababu watataka kuonesha kiwango cha juu. (Sun)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hana mpango wa kumtoa kwa mkopo kiungo Andreas Pereira, 21, baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango katika mechi za kujipima nguvu. (Sun)

*Picha ya Nemanja Matic akiwa amevaa jezi ya Man Utd ambayo imezagaa mitandaoni na kutumika hata na gazeti la Star Sport haijathibitishwa bado kama ni rasmi la halisi.

*Sun Sport ukurasa wa michezo inasema Arsene Wenger huenda akapoteza wachezaji wenye thamani ya pauni milioni 125 bila kupata hata senti kwa kuwa watatu hao mikataba yao inaisha mwakani na wataondoka bure iwapo hawatauzwa msimu huu na ikiwa hawatasaini mikataba mipya.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...