MTEULE THE BEST
Wote tunaijua stori maarufu ya Meli ya Titanic (wengi wetu baada ya kuona movie yake iliyoigizwa mwaka 1997 na waigizaji nyota Leonardo DiCaprio na Kate Winslet). Lakini je Titanic ndio chomb cha majini kilichopata ajali na kuua watu wengi zaidi katika historia?
Jibu ni Si Kweli. Kuna vyombo viwili zaidi vilivyopata ajali zilizoua watu wengi zaidi na vingine zaidi vya kivita(katika Vita ya Kwanza na Pili ya Dunia).
Hivi ni vyombo vilivyopata ajali majini na kuua watu wengi zaidi katika historia:-
1. MV Wilhelm Gustloff (Januari 1945)
Mnamo Januari 1945, Meli hii ya Kijerumani iliyoitwa MV Wilhelm Gustloff ilishambuliwa na torpedo 3(torpedo ni makombora yanayosafiri majini) ikiwa kwenye Bahari ya Baltic wakati ikiwa katika mchakato wa kuwaondoa katika eneo la vita raia, wanajeshi na Maofisa wa Jeshi la Nazi waliokuwa wamezingirwa na Red Army(Jeshi la Urusi) eneo la Mashariki ya Prussia. Baada ya kushambuliwa eneo la upande wa kulia, meli hiyo ilizama ndani ya dakika 45. Takribani watu 9,400 walifariki kwenye ajali hiyo na kuifanya kuwa ajali iliyoua watu wengi zaidi majini ikihusisha meli moja kuzama katika historia.
2. MV Doña Paz (Desemba 1987)
Kivuko hiki cha Kifilipino kilizama baada ya kugongana na meli ya mafuta mnamo Desemba 20, 1987. Kutokana na kusababisha vifo takribani 4,375 ajali hiyo ndiyo iliyoua watu wengi zaidi majini wakati wa amani(usio wa vita). Wakati abiria wengi wakiwa wamelala, kivuko hiki kiligongana na meli ya mafuta iliyokuwa na mapipa 8,800 ya petroli. Mgongano ulisababisha moto ambao ulisambaa haraka hadi kwenye kivuko na kuwasha hadi maji yaliyokuwa yanazunguka. Inasemekana kuwa 'life jackets' zilizokuwa kwenye kivuko hicho zilikuwa zimefungiwa na kuwafanya abiria kulazimika kujirusha kwenye maji yaliyojaa papa na yanayowaka moto ili kujiokoa.
3. RMS Lusitania (Mei 1915)
Meli hii ya Uingereza ilikuwa ikifanya safari kati ya Liverpool na New York ikipitia bandari iliyopo Queenstown(hivi sasa Cobh) Ireland. Kipindi cha Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza, meli hii ilipigwa na kombora la Ujerumani mnamo Mei 7, 1915 na kuzama ndani ya dakika 18.
Ajali hiyo iliua abiria 1,198 kati ya 1,959 waliokuwemo ikiacha manusura 761. Kuzama huku kulibadili mtazamo wa nchi nyingi dhidi ya Ujerumani na ilichangia katika kujiingiza kwa Marekani katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na ilikuwa ikitumiwa kama sababu ya kushawishi vijana kupigana vita.
4. RMS Lancastria (Juni 1940)
Meli hii ya Uingereza ilishikiliwa na serikali kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ilizama mnamo Juni 17, 1940 na kusababisha vifo zaidi ya 40000
5. RMS Empress of Ireland (Mei 1914)
Meli hii ilizama katika Mto wa Saint Lawrence baada ya kugongana na meli iliyobeba makaa ya mawe ya Norway mapema siku ya Mei 29, 1914. Ajali hii ilichukua maisha ya watu 1,012 (abiria 840 na wafanyakazi wa kwenye meli 172). Meli hizi ziligongana kutokana na kuwepo kwa ukungu na kutokana na meli ya makaa kuwa ndogo zaidi, watu waliokuwa upande uliogongwa katika madaraja ya chini walizama papo hapo. Meli hiyo iliegemea upande mmoja haraka sana na kupelekea kukosekana muda wa kutoa life jackets ingawa watu 465 walinusurika.
6. MV Goya (Aprili
Meli hii ya Ujerumani ilikuwa na abiria waliosajiliwa 6,100(na kuna uwezekano wa wengine zaidi wasiosajiliwa) iliposhambuliwa mnamo Aprili 16, 1945 na manowari ya Urusi katika Bahari ya Baltic kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Dakika 7 tu baada ya kushambuliwa meli hiyo ilizama na kuua karibu abiria na wafanyakazi wote wa meli ndani ya meli au nje kwa kuzama au kuganda kwenye maji ya barafu.
Ajali hii inaaminiwa kuwa ya pili kwa ubaya katika historia ya ajali za majini kwa kuangalia idadi ya vifo. Meli ilikuwa na wanawake na watoto wengi na kulikuwa na watoto 2 tu kati ya watu 183 walionusurika.
7. USS Indianapolis (Julai 1945)
Julai 30, 1945 muda mfupi baada ya kupeleka vifaa muhimu vya bomu la kwanza la atomiki la kutumiwa kwenye mapigano kwenda kwenye kambi ya anga ya Jeshi la Marekani ya Tinian. Meli hiyo ilipigwa kombora na Manowari ya Japan na kuzama ndani ya dakika 12. Kati ya mabaharia 1,196 waliokuwemo, 300 walizama na meli.
Takribani 900 waliobaki walikufa kutokana na kukosa maji na kuliwa na papa wakiwa wanasubiri msaada wakiwa katika maboti ya uakoaji bila chakula na maji. Jeshi lilijua kuhusu kuzama huko siku 4 baadaye baada ya manusura kuonwa na mabaharia wa PV-1 Ventura wakiwa wanafanya patrol. Ni mabaharia 317 tu walinusurika.
8. MV Le Joola (Septemba 2002)
Kivuko hiki cha Senegal kinachomilikiwa na Serikali kilizama karibu na ufukwe wa Gambia Septemba 26, 2002 na kupelekea vifo 1,863. Kuzama kwa kivuko hiki ni ajali ya pili kwa ubaya (kwa zile zilizotokea nyakati zisizo za vita) kwa idadi ya watu waliofariki. Kivuko hiki kiliripotiwa kujaza abiria kupita kiasi na kilipokutana na dhoruba kilizama ndani ya dakika 5 tu. Kati ya abiria takribani 2000, ni watu 64 tu walinusurika akiwemo mwanamke mmoja pekee aliyetambulika kama Mariama Diouf aliyekuwa mjamzito wakati huo kati ya wanawake 600 waliokuwemo.
9. SS Mont-Blanc (Desemba 1917)
Meli hii ya Ufaransa ililipuka na kulipua Mji mzima. Ilikuwa imebeba mabomu(vitu vya kulipuka) na kulipuka Bandari ya Halifax mnamo Desemba 6, 1917 na kusababisha mlipuko katika jiji zima la Halifax, Nova Scotia, Canada.
Ikiwa inaingia kwenye Bandari ya Halifax asubuhi ya Desemba 6, iligongana na Meli ya Norway iliyoitwa SS Imo na moto kutokana na mlipuko huo kulipua mzigo wa vilipukizi dakika 20
10. RMS Titanic (Aprili 1912)
Hii ni ajali maarufu kuliko zote. RMS Titanic ilikuwa ni meli ya abiria iliyozama Kaskazini mwa bahari ya Atlantiki mnamo Aprili 15, 1912 baada ya kugonga barafu mida ya saa 5 na dakika 40 usiku ikiwa katika safari yake ya kwanza kutokea Southampton, United Kingdom kuelekea New York, USA.Mgongano huo ulifungua vyumba 5 kati ya 16 vya meli hiyo vilivyokuwa vimetengenezwa kutoruhusu maji kuingia.Abiria na wafanyakazi wa meli walitolewa kwenye life boats ambazo nyingi zilishushwa majini zikiwa hazijajaa watu. Ndani ya masaa mawili na nusu meli ilijaa maji na kuzama. Kabla ya saa nane na dakika 20, Titanic ilivunjika vipande viwili na kuzama ikiwa na watu zaidi ya 1000 ndani. Waliokuwa kwenye maji walifariki kwa kuganda damu kwani maji yalikuwa ya baridi (freezing). [Walioangalia movie ya Titanic wanayajua haya yote
Manusura 710 waliokolewa kutoka kwenye life boats na RMS Carpathia masaa machache baadae. Kuzama kwa Titanic kulisababisha vifo 1,514 na kuifanya kuwa ajali ya tatu kwa ubaya(kwa zile zilizotokea wakati usio wa vita).
11. MV SPICE Septemba 10, 2011
Meli iliyoitwa MV Spice Islander I ya Zanzibar ilizama ikiwa safarini kati ya Unguja na Pemba na taarifa za vifo vilivyotokana na ajali hiyo haziko wazi sana. Makadirio ya mwanzo yalisema vifo vilikuwa takribani 200 lakini baadaye kulikuwa na taarifa kuwa zaidi ya 1500 walifariki.
12:MV BUKOBA MEI 1996

Meli ya MV Bukoba ikiwa Ziwa Victoria wakati ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama.
Usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV BUKOBA ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu.
Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama.
Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.
Mnara wa Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba uliopo Makaburi ya marehemu waliotokana na ajali hiyo, Igoma – Mwanza.
Hakika Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake aliguswa na Msiba huo ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa Wetu, baada ya Meli ya MV.Bukoba Kuzama hatua chache kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea
Mkoani Kagera.
Mkoani Kagera.
Meli ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilizama katika Maji ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza yapata umbali wa kilomita zipatazo 30 kutoka ufukweni mwa maji na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika Meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17. Jambo la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo wa kubeba abiria 430).
Makaburi ya waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Bukoba yaliyopo, Igoma – Mwanza.
Pengine tumezoea kuita kwamba Mei 21 Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzama kwa Meli hiyo ambayo iliigeuza taswira ya Mji wa Mwanza, kwani kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo walipigwa na Butwaa baada ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.

Wakati leo tunakumbuka tukio hili ambalo limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo imani ya watalaamu wa masuala ya usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.

Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri (Picha zote na Maktaba).
Lakini wakati tunatafakari suala hilo, pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe bila kusubiri kusukumwa na mtu hususani wale wenye mamlaka ya kuleta matokeo chanya katika kuboresha hali ya usafiri majini Ikiwemo Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA kwamba tulijifunza jambo lolote kutokana na ajali hiyo ya Mv.Bukoba?
Na Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo jambo hilo? Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu? Je, tumekwisha jijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu?.
Lakini pia wapo waliohoji na bado wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo ya Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo? Lakini pia wakiwa bado wanaendelea kujiuliza ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo? Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha kutokea na kuyagharimu maisha ya Watanzania ikiwemo ile ya mv Spice Ireland iliyotokea Septemba 10 mwaka 2011 katika Mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja Zanzibar.
Lakini yote Tisa, Kumi ni stofahamu iliyoibuka juu ya Chanzo cha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea hapa nchini.Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Wakaguzi wa na Waangalizi kwa maana ya Mamlaka husika, Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Nahodha na Timu yake na wapo waliosema chombo kilikuwa kibovu.
Wapo waliodai chombo hicho kilikuwa kimebeba Mizigo na abiria kuzidi uwezo wake na wapo waliodai kuwa abiria wenyewe walisababisha ajali hiyo kwani walilazimisha kupanda Melini ilihali chombo kilikuwa kimejaa huku mlolongo huo ukihitimishwa na wale waliohusisha ajali hiyo na Imani za Kishirikina.
Mimi nasema sina nia ya kuandika hayo yote kwa lengo la kumtafuta mchawi ila lengo langu ni kuyaweka wazi hayo yote ili kila mmoja kwa namna anavyohusika na anavyoweza kusaidia namna ya kufanya ili kuepukana na ajali kama hiyo ama kama ambavyo wengine husema tusiangalie tulipoanguka bali tuangalie tulipojikwaa.
Wapo wengi waliowapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao na mmoja wao ambae alimpoteza mpendwa wake katika maisha yake ni Mwanamitindo maarufu hapa nchini ambae pia anafanya shughuli zake barani Ulaya Flavian Matata ambae yeye alimpoteza Mama yake mzazi pamoja na binamu yake.
Pamoja na watu wengine, Matata amekuwa na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa kufika Mkoani Mwanza katika eneo la Igoma walikohifadhiwa watu waliopeza maisha katika ajali hiyo ya Mv.Bukoba
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyika kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
BONYEZA HAPA :- KUPATA PESA BURE KWA KUTUMIA SIMU YAKO JIUNGE HAPAambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyika kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
Maoni