02.08.2017
Manchester United wanataka kumsajili beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier, 24, ambaye kwa sasa amepigwa marufuku kuingia Uingereza. (Daily Mirror)
Manchester United wamemuulizia kiungo wa Anderlecht Leander Dendoncker, 22, lakini hawatarajii kumsajili msimu huu. (Manchester Evening News)
Monaco wamepandisha bei ya Kylian Mbappe hadi euro milioni 200 kwa matumaini kuwa Barcelona huenda wakamtaka ili kuziba pengo la Neymar anayedhaniwa kwenda PSG. (Mail Online)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema alizungumza na mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata kuhusu kwenda White Hart Lane, lakini Morata hakutaka kugombania namba na Harry Kane. (Daily Mail)
Arsene Wenger amemuambia mshambuliaji Alexis Sanchez, 28, kuwa hatouzwa kwa klabu yoyote ya England msimu huu. (Times)
Alexis Sanchez amewashawishi wachezaji wenzake kuwa anataka kuondoka Arsenal msimu huu, huku Manchester City na PSG zikiendelea kumnyatia, na kikosi cha Arsenal sasa kinaamini kweli Sanchez anataka kuondoka. (Daily Mail)
Liverpool hawamtaki Rafinha au Andre Gomes ambao wametajwa kuwa katika sehemu ya mkataba wa Barcelona wa kumtaka Philippe Coutinho. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20, anafanya vipimo vya afya ili kujiunga na Leicester City kwa pauni milioni 25. (Leicester Mercury)
Manchester City wamesisitiza kuweka kifungu cha kuweza kumnunua tena Iheanacho. (Daily Telegraph)
Arsenal wanafikiria kumsajili kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 26. (ESPN)
Chelsea wanamnyatia winga wa Inter Milan Antonio Candreva, 30. (Daily Mirror)
Everton wanafikiria kumsajili beki wa Lazio Wesley Hoedt, 23, kwa pauni milioni 12. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Valencia Alvaro Negredo, 31, anakaribia kusaini mkataba kujiunga na Besitkas, licha ya Swansea na Leeds kumtaka. (AS)
Kipa wa Arsenal David Ospina, 28, anapanga kubakia Emirates na kuipigania namba yake. (London Evening Standard)
Barcelona wanataka kumchukua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, au Paulo Dybala wa Juventus kuziba pengo la Neymar. (Independent)
Barcelona watataka kiungo mmojawapo wa PSG – Angel Di Maria, Julian Dexter, Adrien Rabiot au Marco Verratti kuwa sehemu ya mkataba wa kumchukua Neymar. (Mundo Deportivo)
Barcelona wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, 26, kuziba pengo la Neymar. (Cadena Ser)
. Uwe na wiki njema
Maoni