Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Uingereza yawatahadharisha raia wake wanaoelekea Tanzania Aprili 26



Bendera ya Uingereza

Iwapo wewe ni raia wa Uingereza na unapanga kusafiri kuelekea Tanzania wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu ili kuhakikisha kuwa haujipati katika maandamano ya kisiasa yanayopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili .


Katika tahadhari ya usafiri iliotolewa na ubalozi wa Uingereza, wasafiri wameonywa kwamba ijapokuwa safari za kuelekea taifa hilo hazina matatizo yoyote, wageni wanaoingia nchini humo siku hiyo wanafaa kuwa makini kwani iwapo kutakuwa na maandano kunaweza kuwa na 'maafa'.


Kulingana na gazeti la The Citizen Tanzania, tahadhari hiyo ilitolewa kufuatia wito wa kufanyika kwa maandano dhidi ya serikali na mwanaharakati wa mtandaoni anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi.



Anadai kwamba maandamano hayo ni ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.



Barua ilioandikwa na ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari nchini Tanzania

Serikali tayari imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yatakuwa kinyume na sheria.


Rais John Magufuli amesisitiza kuwa maafisa wa usalama watakabiliana na wale watakaoshiriki katika maandamano hayo.


''Kutokana na uzoefu wa hapo mbeleniu balozi wa Uingereza nchini Tanzania umeonya kwamba maafisa wa usalama nchini Tanzania huenda wakatumia vitoa machozi na hata risasi kukabiliana na mandamano yoyote haramu''.


''Kuweni makini mulipo na epukeni makundi makubwa ya watu ama maandamano ya umma'', ilisema taarifa hiyo.


Takriban raia 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila mwaka


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...